Kampuni ya basi la Shabiby, hii ni hatari sana kwa abiria wenu

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama yalivyo mawazo ya baadhi ya wadau, naona huu mgogoro na huyo dereva uliununua mwenyewe! Sijaona sababu ya wewe kuingia kwenye basi ambalo liko tayari kwa safari na maspika yanayo ashiria wewe ni mmachinga!

Wakati mwingine, ni vizuri tu ukaheshimu taratibu zao. Na kama umekasirika sana kwa kudhalilishwa mbele ya mke wako, basi hamia kampuni nyingine! Panda Machame Inv. Nayo yako kama Shabiby tu kwa ubora, nk.
 
Hii comment ndio final say.
Kule machame ndio watakubali?
 
Hiyo spika ilikuwa kubwa kiasi gani mpaka Dereva akutoe Kwa nguvu?

Wakati wa Vurugu mkeo kwanini hakuwajuza kuwa ni mtu wake kweli?

Na alipokueleza utoke kwanini hukumwita Mkeo afuate Pesa nje?

Inaonekana hao watu walikosa uvumilivu ila na wewe ulikosa utulivu wa akili pia. Hili suala halikupaswa kufikia kukamatana mashati kama nyote mngetumia busara
 
Kuna wapuuzi wanasema mleta uzi ana kosa.

Wajinga sana.

Hata kama ni muuza vitu kuna namna ya kumkataza mtu kitu na mkaachana kwa heshima tu.

Ila mleta uzi inaonyesha ulijibu kwa ubabe kwasababu mtu akikukataza kitu na jibu lako likawa kumuelewesha unachofanya sicho anachofikiria hakuna namna huyo mtu atakukunja. Labda akwambie mpe kwa dirishani.

Labda uelezee kabla hajakukunja ulimjibu nini? Haukumuambia kwamba mshahara wake unamlipa ndani ya siku na taa ya gari lako inaweza kumlisha yeye na ukoo wake?
 
Mbele ya mke wake lazima avimbe. Ndio kumemponza huko mpaka kufukuzwa kama kibaka
 
Hizi ni hasira za kudhibitiwa....
lkn kwanini upande na spika sijui maiki kwenye gari ya watu ya biashara.....
 
madhara ya chanjo yameanza mapema
 
Pole mkuu Ila binafsi sipendi mabasi yanayoruhusu hovyo wamachinga na watu ambao sio abiria, inawezekana hukuwa na Nia ya kufanya biashara Ila Kuna kitu hujaweka wazi. Kwa hili shabiby wasilaumiwe saana
 
Nyuma ya basi huwa kuna namba

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Unalalamika sana, kwanini huyo mkeo hakukutetea au kufata hela huko chini?
Naamini ulitangaza humo ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…