Kampuni ya basi la Shabiby, hii ni hatari sana kwa abiria wenu

Eti Hana kadi ya benki, watu wanatumia simbanking tu mie hata sijui kadi ipo wapi?.

Wife aliona huyu bwege wacha wamdunde akajikausha 😃😃😃 wanawake sio watu wazuri 😃😃😃😃😃
 
Hilo Jina lako Jasiri hujalitemdea haki
Mwanaume unakuaje mnyonge mbele ya bebe wako ?
 
Haya maisha ya ajabu sana usikute wakati hayo yanatukia inawezekana mke wako alikuwa anafurahia huku akijisemea wacha wamkoneshe amezidi,Halafu unatembea na spika huwa unauza sumu za mende na panya?
 
Fanya mpango wa namba nimpokee, mimi ni msamalia mwema nipo Dodoma hapa Area D karibu na ofisi za Shabiby
 
Daah!🙄
 
Kama ni kweli kwani nini hukwenda dirishani kumpatia hiyo pesa?
Kama ndivyo kuna Mpesa au Tigo pesa kwanini hukufikiria kumtumia Kwa njia hiyo?
Kwa nini usimpe Dereva ampelekee?au konda!
Kwanini usiache hiyo speaker nje ambayo ilikuweka kwenye mazingira ya kutafsiriwa vibaya?
Kwa kuja kwenye mitandao ya kijamii Ndio suluhisho?
Huna sababu ya kuhukumu wengine Kwa sababu ndogo ndogo hivyo
Jenga utulivu Fanya kazi Kibosho tunahitaji hela December
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema hiyo safari ilikua ya ghafula kiasi cha kushindwa kujipanga kabla ya siku ya safari,halafu mke wako unampatia vijihela kwenye basi badala yeye ndio awe mtunza hazina,ili ikitokea dharula yoyote achukue pesa ila wewe upewe taarifa tu ya matumizi na jinsi pesa ilivyo tumika ua bado hujakomaa,au sio mke wako huyo.
 
Duh[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyu Jamaa anadis shabiby sasa ata support kampuni gani wkt zilizobaki Karibu zote M*vi Tu.
Shabiby sio tatizo,ila huyu dereva,maana hata ushahidi wa sababu ya mimi kuingia ndani ya basi nilimwonyesha,ila hakutaka kunielewa

Hata hivyo mimi ndie nilikuwa namsafirisha mke wangu,

Shida ni huyu dereva,maana ni mteja ambaye nikitokea hapa jijini arusha ,hata wafanya kazi wa shabiby ofisini,wananitambua

Hata tangu nianze ku utumia usafiri wa shabiby,sijawahi na ubaya alio nifanyia

Wakati mwingine ninasafiri na shabiby toka dodoma mpaka tunduma,dodoma arusha,dodoma dar,

Sijawahi kutana na tatizo hili

Ndio maana naishauri shabiby,wamchunguze huyu dereva

Nadhani ana shida
 
Wewe utakuwa kanjanja tu usikute ulikuwa unataka kuwaibia abiria,ilishindikana vipi kumuachia mtu yoyote hilo lispika nje mpaka uingie nalo ndani ya basi hovyo sana wewe.
 
Yaani katka Hali ya kawaida umeenda kutaka kuingia ndani ya Basi, dereva akakukataza (maybe alishaanza kuondoka) Simply ilitakiwa umwite Wife umpe hiyo hela ya matumizi then ushuke story ingekuwa imeishia hapo, sasa inaonekana na wewe ulikomaa tu uingie kilazima huku umebeba mi speaker yako hiyo lazma angekukazia.
Halafu km tatizo ingekuwa dereva Tu na kondakta umesema wanakujua Basi wangekutetea lakini umesema na wao wamechangia kukukunja vizuri na kukudhibiti ili usilete jeuri hii inaonesha ulishaanza kuwa na kiburi na kuleta rabsha hapo kitu ambacho lazma wangekubananisha tu.

Mkuu sehemu Kama zile zingatia Sana "Appearance" ulikuwa ktk mwonekano gani mpk wakashindwa kukuelewa unachowaeleza na kuamua kukudhalilisha??? Kama ulikuwa rafu ktk namna ambayo hata abiria wanakutilia shaka hawatakusapoti kwa shida yako.

Lugha uliyokuwa unatumia kuelezea shida yako huenda haikua ya kistaarabu. Kumbuka ile haikua haki yako we kuingia mana si abiria hivyo ulikuwa ni ombi TU unaomba usaidiwe
Baada ya kushindikana ulitakiwa uangalie option ya pili kumwita wife aje umpe hiyo hela Au hata kumpa konda ampe hapo, hata hii ilishindikana?

Mkuu kwa hicho kilichotokea juu yako peke yake hakitoshi kuwalaumu shabiby na kuwaona hawafai [emoji3].... kampuni hiyo naweza sema ndio pekee iliyokua serious zaidi katika kutoa huduma In a profeshno way sasa we tena unawadis kwa hiyo sababu ndogo TU. We kubali kwamba na wewe una makosa katka hicho kilichotokea na pole kwa inconvenience uliyoipata.
 
Haya maneno ya dharau na kebehi yanashangaza sana.
Kampuni inaweza ikawa nzuri lakini mtu mmoja tu akaichafua.
Kimsingi mleta hoja amedhalilika. Kwanini huyo dereva hakutumia busara kumsikiliza na kumsaidia?
Masala ya kusukumana ni ya kizamani. Kiukweli, baadhi ya wahudumu kwenye mabasi hawatambui wajibu wao kama watoa huduma.
Hali hii ipo na kwenye biashara nyingine. Angekuwa muhusika amevaa suti na Tai asingebughudhiwa. Tujenge tabia ya kuheshimu watu.
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…