Kampuni ya Elsewedy ipo katika mazungumzo kuwekeza katika reli na kiwanda cha mbolea

Wapingapi "mmechambuka chambuka sana"
Kwa kweli awamu hii, lugha ya Kiswahili nayo itaneemeka sana kwa kuongeza misamiati, tulianza na "japo yameregea..", tukaja "wanademka", sasa "chambuka chambuka", na wewe Mkuu Wakudadavuwa , leo umetuongezea msamiati wa "wapingapi"...
Kiswahili kitakuwa, kitanenepa, kitanona na kuzidi kuwa kitamu.
Hongereni.
P
 
Acha uzezeta hapa.
Sio kila chama tofauti na CCM ni chama cha upinzani, vipo vingi sana ni vyama vya upambe wa CCM, na havina hadhi ya kuitwa vyama vya upinzani, havipingi chochote dhidi ya CCM. Rais kukutana navyo ni kutaka kutughalai.

Sote tunajua, upinzani kwa sasa unabebwa na CHADEMA, na Rais anapotakiwa kukutana na wapinzani inamaana akutane na upinzani unaongozwa na CHADEMA. Tofauti na hapo ni upuuuzi mtupu.

Kwanini Samia anaogopa kukutana na CHADEMA?
Kwanini Samia anaogopa wafuasi wa CHADEMA kukutana?
 
Unaongea vitu vya kufikirika, tayari ubongo wako umeshaamini hayo unayoamini, endelea kuyaamini
 
Hamuogopi 'gaidi' Mbowe atalipua hio miundo mbinu?
Mbona tumerekebisha hati ya mashitaka!! Kwa sasa ni uhujumu uchumi, kufadhili vitendo vya ugaidi, kukutwa na silaha kinyume cha sheria, na kukutwa na nguo za jei dabliu tiizedi.

Tuligundua tulichemka kutumia neno "GAIDI" maana Gaidi siyo mtu wa mchezo mchezo! Gaidi anakuripua tu dk 0!
 
We uoni anavyoilipua ccm
 
Unawaamini Mkuu? Si unakumbuka wale wamalaysia waliokuwa wajenge Disney Park Simiyu?

Amandla...
 
😁😁😁 Sikua nimejua Kama amebadilishiwa mashitaka mkuu
 
Mwananchi unataka upate nini wewe kama wewe?Acha watu wawekeze wewe kama umeshindwa kujitafutia ugali,serikali kamwe haiwezi kukupa.
 
Wanataka pia kuwekeza kwenye reli? Sisi tz tusikubali reli binafsi hata treni binafsi. Wawekeze kwenye maeneo kufuatana na mpango wetu sio wao.
 
Wanataka pia kuwekeza kwenye reli? Sisi tz tusikubali reli binafsi hata treni binafsi. Wawekeze kwenye maeneo kufuatana na mpango wetu sio wao.
Kuna tatizo lolote wakiwekeza kwenye reli binafsi? Kama wanajenga kwa hela yao, sie tunawatoza kodi na kuingiza mapato shida iko wapi?
 
"Haya nendeni mkateleze hayo mlosema"
Haha mzee sasa wewe una ushahidi upi kwamba anasemaga hivyo? Pili baraza la mawaziri linakua na agenda na anaziandaa katibu mkuu kiongozi wanakua na rais wameshafanya maamuzi pale wanaenda kujadiliana kwa pamoja kila mtu atoe mchango wake ili zile ajenda ziweze kuwa na manufaa zaidi, kwenye baraza la mawaziri huwa hawaulizi wizara hii mmejipangaje huwa kuna ajenda maalumu
 

..vipo vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikitumika KUHUJUMU ajenda ya mabadilliko nchini.

..sasa serikali izingatie ukweli huo itakapoamua kukutana na vyama vya siasa.

..lakini nakubaliana na wewe kwamba CDM wakubali kukutana na Rais ktk mazingira yoyote yale. Nashauri wasiweke masharti.

..jambo la msingi madukuduku ya vyama genuine vya upinzani yafanyiwe kazi, na HAKI SAWA itamalaki kwa vyama vyote vya siasa.
 
Kuna tatizo lolote wakiwekeza kwenye reli binafsi? Kama wanajenga kwa hela yao, sie tunawatoza kodi na kuingiza mapato shida iko wapi?

..wakijenga kwa fedha zao upo uwezekano wakadai msamaha mkubwa na wa muda mrefu wa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…