Kampuni ya Emirates National Group kutoka UAE kuanza kuendesha mabasi 177 ya BRT Dar es Salaam Januari 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Naona waarabu wanazidi kutambana tu kwenye nchi yetu, kila kitu wanapewa wao sasa.
=================
Kampuni ya Emirates National Group (ENG) yenye makao yake makuu katika Falme za Kiarabu (UAE) inatarajiwa kuanza kuendesha mabasi 177 katika awamu ya kwanza ya Mfumo wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT) wa Jiji la Dar es Salaam ifikapo Januari 2026, serikali imesema.

Mabasi hayo, ambayo yamepangwa kuhudumia njia ya Kimara–Posta–Kariakoo, kwa sasa yako katika hatua ya utengenezaji na yanatarajiwa kuwasili na kuanza kazi mapema mwakani, kwa mujibu wa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa DART, Bw. William Gatambi.

“Tulitarajia mabasi yangekuwa yamewasili nchini kufikia sasa, lakini tumejulishwa kwamba bado yapo kwenye utengenezaji,” alisema Bw. Gatambi. “Hata hivyo, kila kitu kinaendelea vizuri na tunatarajia mradi kuanza Januari mwakani.”

Ujio wa ENG unafuatia makubaliano kati ya serikali na kampuni hiyo ya UAE kuendesha na kusimamia njia za awamu ya kwanza za BRT chini ya mpango wa Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ulioingiwa mwaka huu.

Mwekezaji huyo ataendesha vituo vikuu vitano, vituo vya kati 27, vituo vya matawi manne, na kuajiri madereva wake mwenyewe, hivyo kuchukua nafasi ya mtoa huduma wa muda, UDART.

“UDART ilikuwa mtoa huduma wa muda wakati serikali ikiendelea kutafuta mwekezaji wa kudumu,” alifafanua Bw. Gatambi.

Hatua hii inatarajiwa kurejesha ufanisi wa mfumo wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam, ambao umekumbwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika siku za hivi karibuni.

DART ilisema mapema mwaka huu kwamba mtandao wa BRT wa Dar es Salaam utakuwa na awamu sita, ambapo kila awamu itasimamiwa na mtoa huduma tofauti, na ikahimiza makampuni ya ndani yenye uwezo kujiandaa kushiriki katika uendeshaji wa awamu zijazo.

Screenshot 2025-10-17 182144.png
 
Hii nchi ni vituko tena ni vichekesho, kama Mwendokasi imewashinda tu kuendesha, halafu bado wamekaza mafuvu kung'ang'ania kuendesha vichwa vya Watz milioni kadhaa na ujazo, kama siyo wanagombania nafasi ya upigaji na siyo ustawi wa wanachi ni nini hapo!.
 
Yaani katika waTanzania 60+mil tumekosa wanaoweza kuendesha huo mradi.Hii ni aibu na wala sio jambo lakujivunia.

Hili suala la serikali kushindwa kufanya/kusimamia miradi ya umma inaonesha ni kiwango gani kuna udhaifu mkubwa serikalini.

TTCL hali hairidhishi,Udart nao ndio hvyo tena.Wanaoongoza hii miradi wao wanakuwa matajiri ila miradi inakuwa inafirisika mbona inafikirisha sana.

Mifumo yetu yakupambana na ubadhilifu wa mali za umma haujitoshelezi ndio maana mashirika ya umma yanafilisika ila wanayoyaongoza wananeemeka.

Tuige mfumo wa CCP kwenye kushughulikia wezi wa mali za uuma itatusaidia sana.
 
Naona waarabu wanazidi kutambana tu kwenye nchi yetu, kila kitu wanapewa wao sasa.
=================
Kampuni ya Emirates National Group (ENG) yenye makao yake makuu katika Falme za Kiarabu (UAE) inatarajiwa kuanza kuendesha mabasi 177 katika awamu ya kwanza ya Mfumo wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT) wa Jiji la Dar es Salaam ifikapo Januari 2026, serikali imesema.

Mabasi hayo, ambayo yamepangwa kuhudumia njia ya Kimara–Posta–Kariakoo, kwa sasa yako katika hatua ya utengenezaji na yanatarajiwa kuwasili na kuanza kazi mapema mwakani, kwa mujibu wa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa DART, Bw. William Gatambi.

“Tulitarajia mabasi yangekuwa yamewasili nchini kufikia sasa, lakini tumejulishwa kwamba bado yapo kwenye utengenezaji,” alisema Bw. Gatambi. “Hata hivyo, kila kitu kinaendelea vizuri na tunatarajia mradi kuanza Januari mwakani.”

Ujio wa ENG unafuatia makubaliano kati ya serikali na kampuni hiyo ya UAE kuendesha na kusimamia njia za awamu ya kwanza za BRT chini ya mpango wa Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ulioingiwa mwaka huu.

Mwekezaji huyo ataendesha vituo vikuu vitano, vituo vya kati 27, vituo vya matawi manne, na kuajiri madereva wake mwenyewe, hivyo kuchukua nafasi ya mtoa huduma wa muda, UDART.

“UDART ilikuwa mtoa huduma wa muda wakati serikali ikiendelea kutafuta mwekezaji wa kudumu,” alifafanua Bw. Gatambi.

Hatua hii inatarajiwa kurejesha ufanisi wa mfumo wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam, ambao umekumbwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika siku za hivi karibuni.

DART ilisema mapema mwaka huu kwamba mtandao wa BRT wa Dar es Salaam utakuwa na awamu sita, ambapo kila awamu itasimamiwa na mtoa huduma tofauti, na ikahimiza makampuni ya ndani yenye uwezo kujiandaa kushiriki katika uendeshaji wa awamu zijazo.

View attachment 3490066
Waarabu
 
Hii kampuni toka mwaka juzi tunaambiwa inaanza kazi.
SIjui wanatuonaje.
 
waje tu kikubwa huduma bora, ndugu zangu watz mbona nyie dubai mnaenda kwani wao wamesema nyie msiende kwao kuwekeza? acheni roho za wazanzibar wao kuja tanganyika ni shega tu ila mtanganyika kwenda kwao eti zanzibar ni ndogo mnajazana sana mpaka unajiuliza hivi sisi binadamu huwa tukoje

fuullstop, kwishaa
 
Back
Top Bottom