A
Anonymous
Guest
Nilifanya kazi katika Kampuni ya Erolink Limited kwa takriban miaka mitatu lakini nikiwa hapo moja ya changamoto kubwa ambayo niliiona na nimeona bado ipo ni Muajiri kutowajibika katika kulipa stahiki za michango ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Watumishi wa hapo wanakatwa kila mwezi lakini asilimia kubwa ya malipo hayo hayafiki katika akaunti za NSSF.
Mfano mimi mwenyewe, baada ya kuacha kazi na kuanza kufuatilia mafao yangu, niligundua kuwa kuna michango yangu haikuwa imepelekwa kwa kipindi cha miezi saba.
Nilipozungumza na NSSF wanakurudisha kwa muajiri wako tena kwani unakuta alikuwa hapeleki michango, kwahiyo siwezi kupata na ukirudi ofisini kwake hakupi ushirikiano, ukieendelea kumtafuta hapokei simu.
Kinachosikitisha zaidi ni jinsi wakaguzi wa NSSF wanavyoshindwa kuwajibika ipasavyo kuhakikisha taasisi zinapeleka michango yetu ipasavyo.
Hali hii si kwangu pekee, kuna Wafanyakazi wengi wamekuwa wakikumbana na matatizo kama haya.
Baadhi yao walikuwa wakikatwa pesa za mikopo kuilipa Bodi ya Mikopo, lakini fedha hizo hazifikishwi kwenye taasisi husika, na kuwasababishia usumbufu mkubwa.
Hawa wakaguzi wa NSSF kuna viashiria kama wanashirikiana na viongozi wa hizi kampuni kutunyanyasa mtu, unadai haki yako ambayo unakatwa kila mwezi na unaishia kuambiwa wewe ni msumbufu.
Huu ni uhujumu uchumi lakini NSSF kama taasisi ya Serikali inachukulia poa labda inasubiri mpaka tamko litoke kwa Viongozi wa juu.