Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Watu wa hivi ndio sbb y ccm kushinda chaguzi.

Kama mwekezaji unatakiwa kuriski sana ili upate zaidi. Hapo kwenye milioni moja faida kila siku ni shilingi 25000/-
Kwa siku kumi ni laki mbili na nusu.
Mwezi ni 750000/-
Mtaji wako unabaki vilevile hauguswi hata kidogo.

Pesa za kudownlod hoye
Kutaka hela za haraka. Wao wana uwekezaji gani hadi wakupe faidi hiyo kwa siku? Ngoja watu wapigwe. Wanatuona wajinga tulioweka UTT na kupata faida kidogo kidogo
 
Watu wa hivi ndio sbb y ccm kushinda chaguzi.

ccm itashinda miaka yote
 
Kampuni ya FIC Imenitapeli – Naombeni Ushauri

Ndugu wanajamii,

Nimejikuta katika hali ngumu baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 1 katika kampuni ya FIC, lakini sasa fedha hizo hazipatikani. Nimejaribu kutoa bila mafanikio, na sijapata majibu ya kuridhisha kutoka kwa kampuni husika.

Naomba ushauri wenu:
  1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC? Kama ndiyo, ulitatua vipi?
  2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii? Je, ni vyema kuripoti kwa vyombo vya sheria au kuna njia nyingine za kutatua suala hili?
  3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania? Je, imesajiliwa rasmi na mamlaka husika?
Ningependa kusikia mawazo na ushauri wenu ili kujua hatua gani zichukuliwe katika hali hii.

Asanteni.
Imeisha iyo, na ibaki kama ulivyosema.
 
Wenzenu huko Ulaya, wanacheza sana hiyo michezo lakini kwa hela za ziada. Gamble what you can afford to loose! Huku Bongo mtu anakipato cha kuunga unga eti naye anajiingiza huko; sasa akiliwa ana kuja huku kulia lia eti asaidiwe....Kwa kipato chako pengine ulitakiwa ucheze kwa shs 5,000 tu., nani kakutuma ukacheze kwa milioni na hela zenyewe unaokoteza.....
CHEZENI HIYO MICHEZO KWA HELA NDOGO, UKIPATA SAWA, UKIKOSA BASI... NDIVYO ULAYA WANAVYOFANYA!
 
Screenshot_20250306-151705.png
 
Hakuna njia yoyote rahisi ya kujipatia kipato!! haya ndiyo madhara yake.
 
Watu wameongea humu mpaka midomo imekauka au mpaka waongelee matakoni ndio muelewe.Tena sasa hivi muwe mnatapeliwa na kila mmoja atobolewe na spika yake.
 
Kampuni ya FIC Imenitapeli – Naombeni Ushauri

Ndugu wanajamii,

Nimejikuta katika hali ngumu baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 1 katika kampuni ya FIC, lakini sasa fedha hizo hazipatikani. Nimejaribu kutoa bila mafanikio, na sijapata majibu ya kuridhisha kutoka kwa kampuni husika.

Naomba ushauri wenu:
  1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC? Kama ndiyo, ulitatua vipi?
  2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii? Je, ni vyema kuripoti kwa vyombo vya sheria au kuna njia nyingine za kutatua suala hili?
  3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania? Je, imesajiliwa rasmi na mamlaka husika?
Ningependa kusikia mawazo na ushauri wenu ili kujua hatua gani zichukuliwe katika hali hii.

Asanteni.
Kwani hivi wabongo mbona tunatapeliwaga ki...........a sana.
Yaani ni aibu na huzuni kubwa.
Watu hawajifunzi TU kila siku kilio kile kile.
Nyerere alifanya makosa sana kuchukua uhuru wa kupewa mezani. Angepigana hata miaka mitano TU watu wangekuwa very sharp minded. Lakini sasa sisi ni wazito sana kwenye kufikiria.
 
Ndugu mtoa mada, nimefurahi sana kusikia ivo. Wakati mwingine ukitapeliwa tena usisite tena kushare na siti hakika ntafurahi sana
 
Hivi kwanini hatupendi kujifunza, wamepita kina deci na wengineo, lakini bado hatujifunzi...wajinga ndiyo waliwao
Hela ya kudaunlodi tamu sana hamna mtu mvivu yeyote asiyeitamani hio aina ya pesa.
 
Back
Top Bottom