Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Kuna jamaa nilimwambia kuwa LBL ni sawa na F.I.C akawa mbishi sana mara ooo wametuonesha wamesajiliwa ,nikamwambia hata LBL walikuwa wanasema hvyo hvyo kuwa wamesajiliwa lakin bado walitapeli watu
 
Tena hii wanaijeria wamepiga wengi kuliko hata lbl
LBL wametumia nguvu kubwa na wameingia kwenye msala na serikali pengine hela nyingi sana serikali imezishikilia ila FIC aiseee hata serikali haijui kama watu wamepigwaa na kuna maboss wengi sana wamelia bora LBL ilikuwa makapuku
 
LBL wametumia nguvu kubwa na wameingia kwenye msala na serikali pengine hela nyingi sana serikali imezishikilia ila FIC aiseee hata serikali haijui kama watu wamepigwaa na kuna maboss wengi sana wamelia bora LBL ilikuwa makapuku
Hata humu FIC imepita na wengi , pesa sio rahisi dunia hii
 
🤣kuna polisi mmoja amejiunga anasema wenzake wataona ghafla anakua tajir bahati mabaya mpaka sasa hajui kama mambo yameshaharibia
 
LBL waliambiwa waongeze nusu ya pesa za mitaji yao ili kuactivate account, wajinga waliongeza wakaliwa na hizo
 
Pole sana kwa hali hii ngumu uliyokutana nayo. Hapa chini ni baadhi ya ushauri na hatua zinazoweza kukusaidia:


1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC?


  • Ndiyo, inaweza kuwa tatizo linalowakuta wengine pia. Inashauriwa kujiunga na vikundi vya watu walioathirika na kampuni hiyo. Hii inaweza kuwa njia ya kubaini kama kuna watu wengine waliowekeza nao na wakakutana na changamoto kama hiyo. Kama kuna watu wengi walioathirika, kuna uwezekano wa kuungana na kuchukua hatua za kisheria kwa pamoja.

2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii?


  • Hatua za awali:
    • Hakikisha umepata kila aina ya uthibitisho wa malipo yako kwa kampuni hiyo, kama vile risiti, mkataba, au nyaraka yoyote ya kifedha.
    • Jaribu kuwasiliana tena na kampuni ili kujua sababu ya kucheleweshwa kwa malipo yako. Ikiwa kuna mawasiliano rasmi ya simu au barua pepe, itumie kwa maandishi ili uwe na ushahidi wa mawasiliano.
  • Ripoti kwa vyombo vya sheria:
    • Ikiwa kampuni hiyo haijakupa majibu ya kuridhisha na kuna dalili za udanganyifu, unaweza kupeleka malalamiko yako kwa Tume ya Ushindani wa Biashara (Competition Commission) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hii ni kwa sababu kampuni inaweza kuwa inafanya biashara isiyo halali.
    • Unaweza pia kuwasiliana na Jeshi la Polisi na kuripoti kwa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) ikiwa kuna ushahidi wa ulaghai.
  • Tafuta ushauri wa kisheria:
    • Wasiliana na wakili ambaye ana uzoefu na masuala ya udanganyifu wa kifedha. Anaweza kukushauri juu ya hatua zinazofuata, ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na mamlaka za serikali au kuchukua hatua nyingine za kisheria.
  • Kuweka hadharani tatizo lako:
    • Ikiwa hakuna majibu yanayotolewa na kampuni, unaweza kuzungumza na vyombo vya habari ili kuwajulisha watu kuhusu kampuni hiyo na kuzionyesha changamoto zako, hivyo kuongeza shinikizo kwa kampuni kutoa fedha zako.

3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania?


  • Ili kuhakikisha kama kampuni hiyo ni halali, unaweza kuangalia kama ni iliyoregisteriwa na Mamlaka ya Usajili wa Biashara Tanzania (BRELA). Hii itakupa taarifa kuhusu usajili wake na kama ni kampuni inayotambulika kisheria.
  • Pia, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaweza kutoa taarifa kuhusu kama kampuni hiyo ni halali kwa kufanya biashara za kifedha nchini.

Hatua muhimu za kuchukua:​


  • Hakikisha umepata nyaraka zote muhimu (makubaliano, risiti za malipo, barua za mawasiliano) ili kuwa na ushahidi.
  • Tafuta msaada wa kisheria ili kujua njia bora ya kushughulikia tatizo lako na hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya kampuni hiyo.

Natumaini utapata suluhu kwa haraka.
 
toka mwanzo ulionekana na uliambiwa kabisa ni mchezo wa kubahatisha hivyo ulitakiwa kuwekeza huku ukijua chochote kinaweza kutokea.
halikuwa swala na kuwekeza fedha nyingi ila ni kucheza na fedha kidogo na kuvuna sana.
yupo rafiki yangu yeye imemlipa sana na alibakiza fedha zao tu hivyo anamaumivu lakini angalau anacho alichopata.
tulia jipange upya maisha bado yapo na unacho cha kujifunza mwanaume hajaubwa kulialia unapigwa kesho unapata akili nyingine.
MWENYEZI MUNGU akupe nguvu na maarifa mapya katika kutafuta.
 
toka mwanzo ulionekana na uliambiwa kabisa ni mchezo wa kubahatisha hivyo ulitakiwa kuwekeza huku ukijua chochote kinaweza kutokea.
halikuwa swala na kuwekeza fedha nyingi ila ni kucheza na fedha kidogo na kuvuna sana.
yupo rafiki yangu yeye imemlipa sana na alibakiza fedha zao tu hivyo anamaumivu lakini angalau anacho alichopata.
tulia jipange upya maisha bado yapo na unacho cha kujifunza mwanaume hajaubwa kulialia unapigwa kesho unapata akili nyingine.
MWENYEZI MUNGU akupe nguvu na maarifa mapya katika kutafuta.
Washaifunga rasmi au bado wanakula kula
 
Kampuni ya FIC Imenitapeli – Naombeni Ushauri

Ndugu wanajamii,

Nimejikuta katika hali ngumu baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 1 katika kampuni ya FIC, lakini sasa fedha hizo hazipatikani. Nimejaribu kutoa bila mafanikio, na sijapata majibu ya kuridhisha kutoka kwa kampuni husika.

Naomba ushauri wenu:
  1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC? Kama ndiyo, ulitatua vipi?
  2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii? Je, ni vyema kuripoti kwa vyombo vya sheria au kuna njia nyingine za kutatua suala hili?
  3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania? Je, imesajiliwa rasmi na mamlaka husika?
Ningependa kusikia mawazo na ushauri wenu ili kujua hatua gani zichukuliwe katika hali hii.

Asanteni.
Pole sana ndugu ila haya maswali yote ulipaswa kujiuliza kabla hujaamua kuwekeza pesa zako humo.
 
Wekezeni zingine zimekuja, LBL imewaachia watu madeni waliokopa wanalia na marejesho
 
Back
Top Bottom