Kampuni ya godmark funeral directors watoa ofa ya vifurushi vya majeneza

Kampuni ya godmark funeral directors watoa ofa ya vifurushi vya majeneza

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kama ulidhani vifurushi vya muda wa maongezi na data vinatolewa na kampuni za simu za mkononi pekee, utakuwa unakosea; sasa kuna vifurushi vya majeneza.

Tena si tu vifurushi, bali sasa huduma ya mazishi, kaburi na shughuli nyingine za kuwalaza ndugu waliofariki katika nyumba zao za milele, zimerahisishwa.

Mteja akinunua jeneza mapema kabla ya kifo chake, ana uhakika wa kupata punguzo la bei la hadi asilimia 30, lakini pia atakuwa na uhakika wa huduma nyingine za matengenezo ya kaburi kama atakubaliana na watoa huduma.

“Unajua kila mtu lazima afe na ndiyo maana watu wanaandika wosia,” alisema Macmillan Siraki, mkurugenzi wa kampuni ya Godmark Funeral Directors ya mjini Moshi iliyoanzisha huduma ya vifurushi hivyo vya majeneza.

“Unapanga vitu vyako ukiwa hai. Ukishakufa watu watakupangia. Hawatapanga kama wewe unavyotaka

“Hata jeneza, hakuna atakayekununulia kama ulivyotaka wewe wakati ukiwa hai. Kuna baadhi ya watu hawathamini mtu akishakufa na pengine hata fedha ya jeneza ni ya kwake.

Alisema walipoanzisha huduma hiyo ya punguzo, watu wengi walijitokeza.

Screenshot_20181116-135252~2.jpeg
 
This is totally unacceptable. Kwanini wafanye hivi? Serikali iingilie kati. Hata pale muhimbili yapo wazi lazima wawe na staha hata kama biashara yafungiwe kwa ndani. Tuliofiwa na wapendwa wetu wa karibu vitu kama hivi ni fundamentally wrong
 
Acha uoga wewe, nenda katoe order kabla majeneza hayajaisha. Ukikosa sanduku ukifa itabidi tukutie kiberiti
 
Acha uoga wewe, nenda katoe order kabla majeneza hayajaisha. Ukikosa sanduku ukifa itabidi tukutie kiberiti
Wee mkaldayo tulia acha porojo za kindezi humu. Kwa taarifa yako tunapoelekea kuchoma ndio itakuwa mpango mzima. Itasave nafas ya ardho.

Ila dah naogopaga majeneza na vifovifo sipendi kabisa kuvishabikia japo hatuwezi kuvyeepuka
 
😀😀😀😀

Ukichomwa haimaanishi umesamehewa ule moto wa kuleee, ule upo pale pale.
 
Back
Top Bottom