Kampuni ya kuagiza magari ya Orbit imekwenda kinyume na makubaliano yetu katika ununuzi wa gari

Shida watu wanataka gari chap chap.
Kwamba peleka kianzio M6, urudi nyumbani na IST. Nyingine utalipa mdo mdo within 2yrs.

Bora hizo 2yrs utunze hizo hela mwenyewe tu,
Nunua gari ya hizo million 6 au vumilia ifike 8.5M upate gari zuri la kuanzia maisha utalifurahia kuliko kupewa gari mpya ya kuagiza ila ni kausha damu.
 
View attachment 3056960

Hii ni kampuni inaitwa Orbit Group Limited (Orbittz) inayoagiza magari kutoka nje ya nchi. Biashara hio inahusisha pia kutoa mkopo wa mpaka miaka miwili ili kukamilisha gharama ya gari.

Sasa hawa watu, kuna taarifa wanamficha mteja na wanakuja kukwambia baadae sana ambapo pengine unaweza kufikia uamuzi wa kutolichukua kabisa gari, na huku umeshatanguliza hela ya mwanzo, na ndio hapo matatizo.

Mfano, kuna ishu ilitokea (gari liliagizwa na kufika nchini) ambapo kwa makubaliano ya mwanzo, riba ya mkopo wa gari ilitakiwa iwe asilimia 3 kwa mwezi, kwa mkopo wa milioni 11, mchanganuo waliotoa ni kama huo hapo chini
View attachment 3056964
Ambapo kwa mwezi ningetakiwa nilipe 650,000 tsh. Lakini, gari lilivofika nchini, wakanitaarifu kua riba imebadilika na kua asilimia 4.5 kwa mwezi, wakanipa mchanganuo mpya ambapo ningetakiwa nilipe 830,000 tsh kwa mwezi.

View attachment 3056965
Ukiachilia mbali mabadiliko hayo, taarifa nyingine ni kwamba mkopo ule una gharama yake na pia gari inatakiwa ilipiwe premium, ambayo ikawa kama milioni 1.3 nyingine kutoka mfukoni.
View attachment 3056967

Baada ya kufikia uamuzi wa kukataa mabadiliko haya na kuomba hela niliyolipa awali irudi, ndipo wakaanza kuzunguka. Mara wanasema mpaka gari iuzwe ndio walipe.

Na pia zaidi ya hapo. Wakaendelea kusema kwenye ile hela ya awali. Watakata gharama yao ya kuagiza gari.

Ingawa nilikubaliana na yote hayo. Bado wameendelea kuzunguka na mpaka hivi sasa kuna kesi ya madai inaendelea mahakamaini kurudisha hio hela.

Hivyo huu uzi uwe ni tahadhari kwa mtu ambae yuko kwenye hatua ya kutaka kufanya biashara na hawa jamaa. Jua kwamba sio waaminifu.

Na huu uzi sio kwamba ninaandika kuharibia biashara, hapana. Hii hapa ni screenshot ya chat na namba yao, ambayo pia wameeka kwenye ukurasa wao wa Instagram.

View attachment 3056985
Tujifunze kusoma mikataba na kuielewa. Kitu chochote ambacho ni lazima ama probability (mfano ongezeko la gharama za huduma) lazima kiwepo kipengele kitakachosomeka (i) ghrama za huduma zinaweza kuongezeka kulingana na mabadiliko ya soko la bidhaa/utoaji huduma. Mteja atalazimika kukubaliana na mabadiliko hayo. (ii) Bila kuathiri mkataba na kipengele (i) hapo juu, ongezeko la gharama halitazidi aslimia ! (kadhaa) kutoka katika jumla ya gharama iliyosainiwa wakati wa mkataba (iii) iwapo ongezeko litazidi asilimia tajwa hapo juu, mtoa huduma atalazimika kufidia bila kuathiri utoaji huduma kwa mteja.

Na iwapo mtoa huduma atakiri kwamba hakuna gharama fiche, lazima iwepo kipengele kwenye mkataba kinachozuia ongezeko la aina yoyote ile la gharama. Na iwapo mtoa huduma atakiuka, alazimike kulipa fidia pamoja na kurudisha gharama zote za mteja.

Mkataba unatakiwa uwe win win situation na sio kupelekwa kwa maneno matamu wakati maandishi hayaoneshi
 
Niliusoma mkataba vizuri sana na haya yote hayakusemwa. Ni kwamba hawa watu wamekuja kubadilika kwa maneno makavu bila kufuata mkataba waliouandika wenyewe. Na ingawa wanajua kua wamekosea na wanatakiwa kurudisha hela, ambapo hata mwanasheria wao ambae ndie ameweka mhuru kwenye mkataba amewashauri hilo, wanazunguka zunguka. Ninavosema kua ni matapeli, ni matapeli kweli!
 
Duuh, pole mkuu hao matapeli tafuta tu mwanasheria mzuri maana wamebadilisha makubaliano ya awali wenyewe, haki yako utaipata
 
Niliusoma mkataba vizuri sana na haya yote hayakusemwa. Ni kwamba hawa watu wamekuja kubadilika kwa maneno makavu bila kufuata mkataba waliouandika wenyewe. Na ingawa wanajua kua wamekosea na wanatakiwa kurudisha hela, ambapo hata mwanasheria wao ambae ndie ameweka mhuru kwenye mkataba amewashauri hilo, wanazunguka zunguka. Ninavosema kua ni matapeli, ni matapeli kweli!
Kama hayapo kwenye mkataba, jitahidi uwe na wakiki mzuri asiye na tamaa.

Nimesema kuhusu mktaba kwasababu mkataba ukikufunga sehemu, inabidi utii.
 
View attachment 3056960

Hii ni kampuni inaitwa Orbit Group Limited (Orbit tz) inayoagiza magari kutoka nje ya nchi. Biashara hio inahusisha pia kutoa mkopo wa mpaka miaka miwili ili kukamilisha gharama ya gari.

Sasa hawa watu, kuna taarifa wanamficha mteja na wanakuja kukwambia baadae sana ambapo pengine unaweza kufikia uamuzi wa kutolichukua kabisa gari, na huku umeshatanguliza hela ya mwanzo, na ndio hapo matatizo.

Mfano, kuna ishu ilitokea (gari liliagizwa na kufika nchini) ambapo kwa makubaliano ya mwanzo, riba ya mkopo wa gari ilitakiwa iwe asilimia 3 kwa mwezi, kwa mkopo wa milioni 11, mchanganuo waliotoa ni kama huo hapo chini
View attachment 3056964
Ambapo kwa mwezi ningetakiwa nilipe 650,000 tsh. Lakini, gari lilivofika nchini, wakanitaarifu kua riba imebadilika na kua asilimia 4.5 kwa mwezi, wakanipa mchanganuo mpya ambapo ningetakiwa nilipe 830,000 tsh kwa mwezi.

View attachment 3056965
Ukiachilia mbali mabadiliko hayo, taarifa nyingine ni kwamba mkopo ule una gharama yake na pia gari inatakiwa ilipiwe premium, ambayo ikawa kama milioni 1.3 nyingine kutoka mfukoni.
View attachment 3056967

Baada ya kufikia uamuzi wa kukataa mabadiliko haya na kuomba hela niliyolipa awali irudi, ndipo wakaanza kuzunguka. Mara wanasema mpaka gari iuzwe ndio walipe.

Na pia zaidi ya hapo. Wakaendelea kusema kwenye ile hela ya awali. Watakata gharama yao ya kuagiza gari.

Ingawa nilikubaliana na yote hayo. Bado wameendelea kuzunguka na mpaka hivi sasa kuna kesi ya madai inaendelea mahakamaini kurudisha hio hela.

Hivyo huu uzi uwe ni tahadhari kwa mtu ambae yuko kwenye hatua ya kutaka kufanya biashara na hawa jamaa. Jua kwamba sio waaminifu.

Na huu uzi sio kwamba ninaandika kuharibia biashara, hapana. Hii hapa ni screenshot ya chat na namba yao, ambayo pia wameeka kwenye ukurasa wao wa Instagram.

View attachment 3056985
Pole sana mkuu!

Asante pia kwa taarifa. Itawasaidia wengi.
 
pole mkuu.ulitaka sana kujkwamua na adha ila hawa matapeli mim pia kipind nataka gari nilikua interest nao kumbe ndio janja janja yao. bora pbz unanunuliwa chombo pnz islamic unalipa hela wanakua kama wamekuuzia wao . au unatafuta gar kutoka kwa ndugu wa karibu sio dalali
 
mnamuandama sana mleta mada wakati watu wengi tu wananunua magari kwa style ya mikopo umiza kama hiyo ndiomaana vikampuni uchwara vya kulipia kidogo kidogo vinaongezeka kila siku.

Wengi ni wajanja wananja na kesi ziko nyingi sana kuna jamaa yangu yeye alitaka Prado 120 akatanguliza 27 ila mpaka leo gari hana na kesi inazungushwa tu mahakamani.
 
Mimi ninachojua fedha tu ndio hukopwa. Hayo mambo mengine ni kutafuta migogoro anyway pole kwa yote pambana warudishe fedha yako
 
Umefanya vzr kiongozi kutoa ALET kwa wateja wengine wanao taka kufanya bznes nao. Vikampuni vingi vya wazawa wababaishaji MNO!! Sio kwenye magari tu na wengine.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
maneno tu hayo hata kwenye kanga yapo. sa hv ukiwa na m4 cash unapata gar imenyooka kabisa

Na kwanini uhangaike kununua gari kama uwezo hujafikia. Mbona sisi tunapanda daladala na mwendokasi bila shida yoyote. Siku tukipata uwezo tutanunua hayo magari.​
 
Back
Top Bottom