DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 84
- 118
Kampuni ya KEDA (T) Ceramics Co. Ltd imefanya uzinduzi wa awali wa kuwasha mitambo ya kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani, leo Agosti 19, 2024.
Uzinduzi huo umefanywa na baadhi ya viongozi wa Kampuni pamoja wa Wafanyakazi wao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ceramics Co. Ltd, Wayne Zhong.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi huo, Wayne Chong amesema moja ya faida ya mradi huo ni kutoa ajira kwa Wazawa na kutumia malighafi nyingi kutoka Tanzania, akitoa mfano kwa kusema Watanzania wanaotarajiwa kuajiriwa kiwandani hapo ni zaidi ya 5000.
Sherehe hizo zimeendana na hatua mbalimbali za Kitamaduni zilizofanyika kabla ya kuanza kwa zoezi hilo ikiwemo kuwasha moto.
“Uwashaji huu wa mitambo utaendelea kwa majaribio na kumaanisha tupo tayari, hivyo, siku 25 zijazo tunatarajiwa kuzindua rasmi kuanza kwa kiwanda hiki.
“Tumefanikiwa pia kutokana na uwepo wa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutupa ushirikiano, wamewezesha wawekezaji kuendelea kuja Tanzania kwa kuwa kuna fursa nyingi zinazopatikana.”
“Tunaamini tutatengeneza bidhaa bora na zitapatikana kwa bei rafiki kwa wanaohitaji.”
Upande wa Afisa Biashara na Mahusiano wa Twyford Tanzania, John Chimwejo amesema “Tunatarajia kufanya ufunguzi wa kiwanda rasmi na kioo cha kwanza kitazalishwa Septemba 2024.
“Pia malighafi nyingi ambazo tunazitegemea zinatokea hapahapa Tanzania, jambo ambalo ni fursa kwa Watanzania wenzetu kutumia nafasi hiyo kukuza biashara zao, kwani ni Asilimia 18 au 20 tu inayotoka nje.”