Kampuni ya Mabasi ya Ally's Star acheni utepeli

Kampuni ya Mabasi ya Ally's Star acheni utepeli

why?

Member
Joined
Jan 22, 2016
Posts
35
Reaction score
48
Leo tar. 05 July 2024

Katika hali isiyo ya kawaida nikiwa eneo la tukio (nilimsindikiza ndugu yangu ambae nae ni muhanga wa hii habari) abiria waliotakiwa kusafiri na gari kampuni ya ALLY'S STAR T644 kutokea DAR ES SALAAM (Urafiki) kuelekea MWANZA walikumbwa na sintofahamu baada ya kubadilishiwa gari na kuelekezwa wapande gari T944

1. Kwanza gari zote mbili zilikuwepo zimepaki hapo hapo pamoja

2. Wahudumu wawili waliwekwa wasimame mbele ya kila gari kuficha abiria wasione plate number🤣

3. Abiria akija anaambiwa aonyeshe meseji ya tiketi na anaoneshwa gari ya kupanda

4. Baada ya abiria kuingia ndani wakaona gari imechoka, haina mwonekano waliotarajia au kuzoea kwa VIP LUXURY BUS, hapo ndipo abiria waliposhitukia mchezo na vurumai kuanza

5. Wengine waligoma kusafiri na kudai warudishiwe nauli, na wengine kulazimika kuendelea safari kutokana na umuhimu au ulazima wa safari zao

Baada ya kuzungumza na Wahudumu majibu yalikuwa hivi:
1. Baadhi ya Wahudumu walijibu kuwa basi husika ni mbovu ndio maana wamepewa basi ili ratiba ya safar isibadilike. Ilichekesha🤣 kwakuwa basi wanayosema mbovu ipo pembeni na ni nzur kwa mwonekano ndani na nje, inapakia abiria, na ndiyo iliyoanza kuondoka (hii ilikasirisha zaidi abiria🤣🤣)

2. Muhudumu mwingine alijibu kuwa lilikuwa tatizo la booking system ilidisplay bus namba tofauti na iliyotakiwa 🤣🤣

3. Kwakifupi majibu yao yalikuwa ni ya kujichanganya tu

MWISHO
1. Gari iliondoka kwa kuchelewa mida ya saa 11 jion tofauti na muda pangwa 1630HRS

2. Abiria waliokuwa wabishi au waongeaji wakidai haki yao walikuwa wanaitwa pembeni sijui walizungumza nn. Na inasemekana wabishi zaidi ambao walikuja mapema walibadilishiwa gari na kupelekwa kwenye gari waliyokatia tiketi awali

3. ABIRIA wengi walilaani na kusema kuwa hawatapanda tena mabasi ya ALLY'S STAR, kwani basi walilopewa haliendani TSH. 78,000 na wengine walipiga simu LATRA ila sikufanikiwa kfahamu mrejesho

4. WITO kwa wamiliki wa mabasi kuweni smart kwenye management ya biashara za usafirishaji katika zama hizi za utandawazi na ushindani wa biashara, ACHENI JANJA JANJA MNAWEZA POTEZA ABIRIA KWA UZEMBE

5. Au inapotakiwa kutoa maelezo kwa abiria toeni maelezo yaliyo nyooka

6. CC:

  • LATRA
  • Wahusika wa ALLY'S STAR
  • Kampuni zote za usafirishaji abiria

Nawatakia abiria wote wa ALLY'S STAR safari njema na poleni kwa changamoto

Screenshot_2024_0705_182833.png
 
Back
Top Bottom