KERO Kampuni ya Mabasi ya Shabbily line acheni tabia hii haraka, mtazika wengi kuelekea 2025

KERO Kampuni ya Mabasi ya Shabbily line acheni tabia hii haraka, mtazika wengi kuelekea 2025

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huu ni mfano mzuri wa hali ya kushangaza katika usafiri wa umma! Kuendesha basi kutoka Mbeya hadi Dodoma na kurudi tena siku hiyo hiyo ni kazi ngumu sana. Inashangaza kuona dereva anafanya safari hizo mbili bila kuchoka au kupumzika. Kwa kawaida, magari kama haya yanahitaji madereva wawili ili kuboresha usalama na faraja ya abiria.

Maswali kama, "Je, dereva hawachoki?" na "Gari hilo kwanini lisiwe na madereva wawili?" yanatoa mwanga juu ya changamoto na hatari zinazoweza kutokea katika usafiri wa barabarani.

Inaweza kuwa ni mfumo wa usafiri usiozingatia umuhimu wa mapumziko ya madereva, hali inayoweza kusababisha ajali.

Kwa hivyo, ni muhimu kuzingatia usalama na afya ya madereva ili kuhakikisha usafiri mzuri na salama kwa abiria wote.
Una hoja nzuri sana.

Madereva wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha tunasafiiri salama.

Hoja yako ni muhimu kuzingatiwa
 
Ili ushahidi utoshe unahitaji nini!
Au unahitaji maelezo Gani?
Namba ya gari, jina la dereva na namba yake ya simu ikiwezekana na namba yake ya leseni, siku na muda aliyoondoka Mbeya, siku aliyofika Dodoma na muda wa kufika, siku na muda aliyoondoka Dodoma kurudi Mbeya, na muda na siku aliyofika Mbeya kutoka Dodoma

Karibu kutoa ushahidi.
 
Hio ni cha mtoto, Ingawa mabasi ya ABC ya Dr-Tunduma mara nyingi yanakuwaga na madereva wawili lakini kuna siku nimesafiri jioni kutoka Tunduma na gari Ina dereva mmoja ambaye alikua ametoka nayo Dar seku hio pekeake. Alafu mwamba yuko fresh hata hajali!
 
ya gari, jina la dereva na namba yake ya simu ikiwezekana na namba yake ya leseni, siku na muda aliyoondoka Mbeya, siku aliyofika Dodoma na muda wa kufika, siku na muda aliyoondoka Dodoma kurudi Mbeya, na muda na siku aliyofika Mbeya kutoka Dodoma

Karibu kutoa ushahidi.
Ukihitaji ushahidi piga 0673616161 utanikumbuka!
 
Iko hivi. Dereva akipumzika au wakiwa wawili basi mshiko unapungua ila dereva akienda ruti nzima na kurudi anakuwa na mshiko balaa. Tatizo siyo mmiliki wa mabasi bali madereva wenyewe. Labda kuwasaidia ni kutunga sheria hakuna dereva day worker, wawe na ajira za kudumu hapo inawezekana kuachiana shift. Ila kwa sasa sahau kabisa, hakuna dereva atakayeyaka kuachia hela.
kwani wanalipwa shs ngapi per trip?
 
Siku yatakukuta, watakupeleka kuwa omba omba au mauti
Gari haija tengenezwa ili ipate ajali.......wapo madereva tunaomudu masafa.....Kuna watoto tumewafundisha kazi wanatembea Dar...... Juba ...Dar Lubumbashi ,,,,,,,,,Kuna 'Issa dogo''.....anapiga Dar Kigali,,,,,,na hawadeki na hawajapata ajali hawajahi kumvunja ntu hata kidole..........
 
Shida ni madereva wenyewe na tamaa zao, wanataka kibunda cha iende irudi chote akiweke kibindoni.
 
Back
Top Bottom