Kampuni ya Maxcom Africa PLC, wamezidi kuboresha huduma zao

Kampuni ya Maxcom Africa PLC, wamezidi kuboresha huduma zao

dlazari

Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
74
Reaction score
30
Kampuni ya Maxcom Africa PLC, wamezidi kuboresha huduma zao.

LEO wametangaza Huduma zao Mpya ambazo zinaweza kupatikana kwa Mawakala wa Maxmalipo Popote.

Huduma hizi zimeambatana na huduma zilizopo kwenye mfumo wa serikali wa malipk Kielektroniki yaani GEPG.

- Malipo ya bili za Maji mikoa mbalimbali
- Malipo ya Faini za Polisi
- Malipo ya Ada za Vyuo
- Malipo ya Ada na tozo za TRA
- Malipo ya Uhamiaji/Imigration
Nk.

Huduma hizi zote zinapatika a kwa mawakala wa Maxmalipo Popote nchini.

 
Huduma ya malipo ya LUKU mbona sijaiona.
 
LUKU ipo. Hizi zilizoandikwa ni huduma Mpya zilizoongezeka
 
BASI IYI MAXIMALIPO NILISOMA MAXIMELO
 
Page 1 of 2

11 Septemba 2018

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya Maxcom Africa PLC – Maxmalipo inapenda kuutaarifu umma
kwamba, imeongeza huduma mbalimbali kupitia kwa mawakala wake wote
wa Maxmalipo.

Mawakala wa Maxmalipo kote nchini wanaweza kulipisha huduma nyingi
zaidi kutokana Maxmalipo kujiunga na mfumo wa Serikali wa malipo
kielektroniki yaani GePG kupitia kwa wabia mbalimbali.

Huduma hizo mpya zinajumuisha:-
1. Malipo ya Faini za makosa ya Barabarani (Traffic offence) -
POLISI
2. Malipo ya Kodi za TRA (Property Tax)
3. Malipo ya Bili za Maji kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa,
Mwanza, Moshi, Arusha, Makambako, Shinyanga,Singida,Dodoma na
Songea
4. Malipo ya Tozo za Uhamiaji (Immigration)
5. Malipo ya RITA
6. Malipo ya Ada za vyuo na mikopo;
- Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM)
- Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM)
- Chuo kikuu Muhimbili (MUHAS)
- Chuo kikuu Huria (Open University)
- Chuo Cha ufundi Arusha (ARUSHA TECH)
- Dar es Salaam Computing Center (UCC)
- Bodi ya Mikopo (HELSB)
Mwananchi yeyote anaweza kulipia huduma hizi mpya popote alipo wakala
wa Maxmalipo, kwa kuwasilisha nambari ya kumbukumbu na kiasi cha fedha
taslimu anazotakiwa kulipia.


Page 2 of 2
Maxmalipo tunatoa wito kwa Umma kuendelea kujipatia huduma za malipo
kielektroniki kupitia mawakala wetu popote walipo nchi nzima.

Uboreshaji wa huduma za Maxmalipo unaenda sambamba na upanuzi wa
wigo wa utoaji huduma kielektroniki ambao unalenga kuhakikisha Wananchi
wanafikiwa na huduma hizo popote walipo (financial Inclusion).

Ni jukumu letu Maxmalipo kuendelea kutoa huduma bora za malipo
kielektroniki kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuboresha maisha ya na
kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma
Maxcom Africa PLC
________________
Bw. Deogratius Lazari
IMG-20180911-WA0002.jpg
IMG_20180911_190809_968.jpg
 
Back
Top Bottom