Kampuni ya Mtandaoni ya LBL inayojihusisha na matangazo ya biashara siyo Utapeli?

Status
Not open for further replies.

Ditex

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
284
Reaction score
887
Habari wadau wa JF, kuna mtu wangu wa karibu kanitumia huu ujumbe , ananishawishi nijiunge ili nami nipate kipato cha ziada.

Swali, je hii sio scam kweli? Kwa wanaofahamu naomba mnipe elimu

Leo burnett London (LBL) wanakupa task mbalimbali ikiwemo hii ambayo unatakiwa kutazama movie na kuzitolea review ambapo utalipwa kutokana na movie ulizoangalia.

Kabla hujaanza kazi unatakiwa kuweka kiasi cha pesa ambacho kinaanzia Tsh. 50,000 kwa level ya chini mpaka mpaka Tsh. 540,000 kwa level ya juu, na mapato yako yataenda kutokana na kiwango ulichoweka pesa.
 
Keusi kekundu..!!
 
Naijua Leo Burnett tu na hiyo London sio jina kamili ya hii kampuni kwa hiyo ni scam
Kama ni wewe unaeitangaza nakushauri uache kabisa
Kwa jinsi ulivyoweka sifa zote hizo inaonekana ni wewe kabisa unai promote
Kama sio kweli nisamehe
Kama mtu unauliza kitu unashusha sifa zote hizo za nini?
Kwanini usiulize tu je ni Legit au la?
Hawa leo ni scammers wakubwa na wengi wametumbukia humo
Jamani kwa ushauri tu ukiona kampuni au jina la biashara kwanza kabisa ingia google hakikisha Kama ni matapeli au ni kampuni iliyosajili kisheria na iko wapi na pia angalia simu je zinauioano?

Tahadhari kabla ya kupigwa, ni ushauri tu
 
Jana kuna mtu kaniambia hii habari kwa maelezo yake anasema hela anapata kweli ila sikumzingatia sana mana najua wengi wa hivi ni matapeli.
 
Ngoja nikuelezee hii kampuni ya LBL siwezi sema moja kwa moja kua mi matapeli lakini kumesha wahi tokea kampuni nyingi za namna hii kama kalybder, sme na zingine nyingi. Kampuni hizi hua zina dumu kwa miezi fulani 3 mpaka 6 baada ya hapo hutoweka na fedha za watu wengi so cha msingi ukisikia we jiunge mapemaaaaa ili upige zako pesa alafu ukishatoa faida yako kaa pembeni maana hua zinakuja kutoweka baadae, mfano mimi nimeanza hii lbl toka mwezi wa 10 na ninafaida nyingi t lakini najua muda si mrefu watu wanaenda kulia , kwahyo ndugu yangu akili ku m kichwa
 
Safiii
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…