Kampuni ya MYSOL acheni kututapeli wananchi wanyonge

Kampuni ya MYSOL acheni kututapeli wananchi wanyonge

Joined
Jan 30, 2023
Posts
89
Reaction score
284
Hii ni kampuni inayokopesha Sola kwa matumizi ya nyumbani vijijini. Walikuja huku Nyamanoro na kuweka matangazo yao. Kwenye maelezo ya mdomoni wanajua kushawishi, sasa ukiwalipa Pesa ya kianzio kuja kukufungia Sola mpaka uwalipe Pesa ya Mafuta na wanakuja kukufungia wanapojisikia wao.

Sola zao wakikufungia leo baada ya siku mbili zinazima. Hapo utapigwa danadana mwezi mzima hawaji kurekebisha na wakati mwingine simu hawapokei. Natoa tahadhari kwa Wananchi wengine maeneo yote nchini WASITHUBUTU KUKOPA SOLA kwenye hii Kampuni ya MYSOL ni MATAPELI NA MAJIZI watakuja kujuta.

Mimi na Wananchi wenzangu tumekoma,na leo tunaenda Mahakamani kuishtaki Kampuni hii ya KITAPELI
 
Chukua Solar kutoka kampuni ya Sunking ni kampuni ya uhakika pia ni huduma zao ni nzuri na wanabidhaa nyingi zaidi ya Solar. Karibu sana Sunking
 
Kuna sunking sijawahi sikia ukorofi ila pia kuna ZOLA nao wanajitahidi kuwasikiliza wateja wao mimi ninatumia ZOLA na Deni lao nishamaliza na hakuna usumbufu wowote ule ulio wahi jitokeza nina miaka minne sasa sina mawazo.
 
Bei zao zipoje kiongozi?
Ok hawa ZOLA gharama zao ziko juu kidogo lkn sio sana
Mfano mtambo wa zola wa tv inchi 24 mpya pamoja na taa zake zinakuwa tano kuanzio hua ni Tsh 160,000 /= na Mkataba ni miaka miwili malipo yanakua aidha kwa kila siku au mwezi kama kila siku ni Tsh 2000 au kama mwezi hua ni 58,500/=

Namba zao za mawasiliano ni hizi hapa mkuu kwa taarifa kamili kutoka kwao
074-698-5720.
080-071-2222.
Nakushauri tumia za juu hizo kama una muda wa maongezi hizo za chini ni bure lakini zina usumbufu kidogo.
 
Hii ni kampuni inayokopesha Sola kwa matumizi ya nyumbani vijijini. Walikuja huku Nyamanoro na kuweka matangazo yao. Kwenye maelezo ya mdomoni wanajua kushawishi, sasa ukiwalipa Pesa ya kianzio kuja kukufungia Sola mpaka uwalipe Pesa ya Mafuta na wanakuja kukufungia wanapojisikia wao.

Sola zao wakikufungia leo baada ya siku mbili zinazima. Hapo utapigwa danadana mwezi mzima hawaji kurekebisha na wakati mwingine simu hawapokei. Natoa tahadhari kwa Wananchi wengine maeneo yote nchini WASITHUBUTU KUKOPA SOLA kwenye hii Kampuni ya MYSOL ni MATAPELI NA MAJIZI watakuja kujuta.

Mimi na Wananchi wenzangu tumekoma,na leo tunaenda Mahakamani kuishtaki Kampuni hii ya KITAPELI
Nilianza kupata machale Kampuni ilipopiga u-turn ghafla na kubadilisha jina
 
Bei zao zipoje kiongozi?
Ila ushauri wa ziada kama utahitaji kukopa huo mtambo basi jitahidi wakati wa marejesho uwe unarecord kila jumla ya pesa zako unazo zitoa kwao hii inasaidia hata siku ukipewa bili tofauti na ilivyo lipa au Deni kuongezeka kwa bahati mbaya unawaambia na wanakuelewa

Nilipata changamoto hiyo nililipa ilipo fika bado 7000 nikawapigia kuwauliza wakasema bado 68000 lkn nilipo wapa records wanakubali nikawalipa 7000 yao mtambo wakaufungua maisha yanaendelea

NB kila mwezi wanakurushia jumla ya pesa yako ulio lipa na Deni lililo bakia.
 
Mimi ni mteja wa mysol sijawahi kupata usumbufu wowote kutoka kwao wala huduma zao, ila ninachoona watu wengi hua hawasomi terms and condition wanaishia ku sign tu bila kujua wame sign nini kwenye mkataba! Tatizo la solar kuzima ina maanisha hujalipia huduma na muda unavyo zidi kwenda deni linaongezeka hivyo badala ya kulipa pesa ulio ilenga yenyewe ina kujumlishia na siku zilizofuata cha msingi hua ina count down deni husika hivyo ni wewe na uhitaji wako! Nimeongelea uzoefu wangu na bado naedelea kulipia japo siitumii ipo store nimebakiza kama laki3 nikimaliza naiuza maana nimesha pata umene! Tv na taa zake, panel na battery
 
Mimi nilichukua mtambo wa kwanza wa watts 120 mwaka 2020 kwa mwaka mmoja na 2021 nikawa nimemaliza kulipa na haujawahi kunisumbua hata kidogo na napata umeme wa uhakika
Kutokana na kuvutiwa na huduma yao mwaka jana nilichukua tena mtambo wa pili lakini pia sipitii changamoto yoyote mpaka leo,tunapokuwa tunalaumu Mysol tuwe tunaeleza na mazingira halisi yaliyo nyuma ya pazia yawezekana wateja wenyewe ndio tatizo
 
Hao jamaa hawana usumbufu kabisa zaidi ya kulipa tu! Kingine kinachoweza kukupa usumbufu kama wa huyo ndugu hapo juu! Ni upande wa mafundi, ukihitaji fundi wa bei rahisi ndio shida yaani fundi anakupa kijana wake aka saidia fundi hapo ndipo utakutana nao hao vichwa kuuma! Tofauti na hapo hawana ishu! Na mambo mengi kwenye mtambo wao hauitaji fundi kabisa labda kuseti ile panel juu ya bati bhasi! DAWA YA DENI NI KULIPA
 
Nimewai kuwa mtendaji mkuu ktk kampuni hyo kabla ya kubadilishwa jina na kuw mysol mwanzo mobisol baada ya kuondoka kwangu kampuni hyo imeyumba na kuwa ya kizushi Zaid

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kama huu ni mwandiko wa aliyewahi kuwa mtendaji mkuu wa hiyo kampuni, basi nachelea kusema ni kampuni ya kipumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom