Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kaloleni kilichopo Kata ya Janga, Ahmed Kilindo amesema kampuni ya OYA Microcredit imetoa mchango wa shilingi milioni moja (Tsh.1,000,000/=) kwa familia ya Juma Said Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo walioenda kudai sehemu ya mkopo waliomkopesha mke wa Juma.
Kilindo amesema kampuni hiyo imetoa fedha hizo kama sehemu ya pole kwa familia huku akieleza kuwa uongozi wa kampuni hiyo umesikitishwa na kitendo kilichofanywa na wafanyakazi wake kwani ni kinyume cha miiko na maadili ya kazi yao.
Soma Pia:
Aidha Juma amezikwa katika Makaburi ya Mtongani kwa Domo yaliyopo Mlandizi.

- Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa
- Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji
- Mfahamu Juma Jangalu anayedaiwa kuuawa na wafanyakazi wa OYA
Aidha Juma amezikwa katika Makaburi ya Mtongani kwa Domo yaliyopo Mlandizi.