Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo

Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo

Kwa Yeyote aliyesoma Kitabu Cha The Charismatic Charlie Wade atakuwa amesoma matukio kama Ya OYA kwa microcredit za Huko China.

Kwa mujibu wa kitabu kile ukikopeshwa ukashindwa kulipa wanakujeruhi na hata kukuua.

Endapo OYA wana mkono wa mchina....
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kaloleni kilichopo Kata ya Janga, Ahmed Kilindo amesema kampuni ya OYA Microcredit imetoa mchango wa shilingi milioni moja (Tsh.1,000,000/=) kwa familia ya Juma Said Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo walioenda kudai sehemu ya mkopo waliomkopesha mke wa Juma.

Kilindo amesema kampuni hiyo imetoa fedha hizo kama sehemu ya pole kwa familia huku akieleza kuwa uongozi wa kampuni hiyo umesikitishwa na kitendo kilichofanywa na wafanyakazi wake kwani ni kinyume cha miiko na maadili ya kazi yao.

Soma Pia:
Kilindo ameeleza hayo wakati akitoa salamu za uongozi wa eneo hilo kwa familia ya Juma.

Aidha Juma amezikwa katika Makaburi ya Mtongani kwa Domo yaliyopo Mlandizi.
Wangetafuta mwanasheria wawafungulie kesi ya madai wadai fidia kwa kampuni ya oya, maana kampuni kisheria inawajibika kwa makosa ya mfanyakazi ambayo yamefanywa akiwa anatekeleza wajibu wa kazi yake
 
Kwa Yeyote aliyesoma Kitabu Cha The Charismatic Charlie Wade atakuwa amesoma matukio kama Ya OYA kwa microcredit za Huko China.

Kwa mujibu wa kitabu kile ukikopeshwa ukashindwa kulipa wanakujeruhi na hata kukuua.

Endapo OYA wana mkono wa mchina....
Tuko kwenye mfumo wa kikatili
Watu nao wanakuwa makatili

Ova
 
Back
Top Bottom