Kampuni ya rifaro imekufa

Kampuni ya rifaro imekufa

ni bora pesa yangu nikale masanga kuliko kupoteza muda kwenye networking business,

hawa jamaa kama ndo siku ya kwanza unaingia kwenye mkutano wao mama yangu unatoa pesa. mi nilipelekwa siku moja ukumbi flan hv pale ITV mwenge, daaah kuna kadada kanatoa ushuhuda kalikuwa chuo baada ya mwaka mmoja kameanza kuingiza million 2 kwa mwezi kameshanunua gari ya kutembelea. nikasema C'EST LA VIE

walichoharibu ni kuniambia kiingilio 350,000 halafu unapewa midawa uuze kama machinga halafu bei juu labda wanunue wabunge na watu wa masaki, oysterbay huko.

jamaa angu hadi tunamaliza chuo maskini hata kununua smartphone ya forever living hajawahi.
 
Jamani vp kuhusu forever product maana kuna mtu ananishawishi sana niingie lakin roho yangu inakataa..Naomba ushauri wadau
Ss km roho inakataa si uache?!

Mi sifanyi bness zao sitaki!
Ila natumia bidhaa zao ,hasa dawa ya meno,ni nzuri japo ni ghali!
 
Ubishi mbaya sana kunajamaa yangu tumesoma naye nilimwambia kuwa wale ni kama deci tu mpaka alinichukia lakni mpaka mda huu atakumbuka ushauri wangu.
 
Bora nitembeze ubuyu wa zenj hela naiona kuliko huu ujinga!
 
kuna jamaa yangu alinishauri sana nijiunge na kampuni ya rifaro kipindi inaanza, leo nimemuuliza kafikia wapi ananiambia kampuni imekufa natumia fursa hii kumpa pole yeye na wale wote waliojiunga na hii deci pia kama angalizo ukiona kampuni yoyote ya network marketing ujue ni utapeli tu wanachogeuza ni bidhaa na mbinu ila rengo ni lilelile kuuza watu biashara ikiwa satured vizazi haviongezeki wanaingia mitini.
KWENYE MAGROUP YA WATSUP HIVI SASA
KUNA UPUUZI HUU MWINGINE NIMESHAUSHITUKIA LAZIMA TU UTAWALIZA WATU HAPO BAADAEE.

Plz Wadau kuweni Makin na hii kitu, Usidanganyike na Mahela Meengiii wakat yeye mwenyewe hana kitu.

[11/3, 18:26] [emoji383][emoji387]Administrator[emoji385][emoji383]: [emoji269]TENGENEZA 1,920,000 KWA MTAJI WA SHILING ELFU 1 (Tsh 1,000).

Karibuni katika fursa inayoitwa "PAYS4EVER"

*SOMA MAELEZO YA HII FURSA KWA UMAKINI AFU KAMA HUJAELEWA ULIZA MASWALI*

_PAYS4EVER_ Ni mfumo unaowezesha watu kuchangiana michango ya hiari moja kwa moja bila kuhusisha mtu wa kati kwenye akaunt zao za simu au za benki kulingana na uamuzi wa mwanachama.

[emoji269]PAYS4EVER INA MFUMO WA 4X3 MATRIX (YAANI UNAWASHIRIKISHA WATU WANNE NA UTAPANDA MPAKA DARAJA LA 3 AMBAPO KILA DARAJA UTAJITENGENEZEA FAIDA

*MCHANGANUO WA MICHANGO PHASE 1*

✍Unajiunga kwa Tshs.1,000 na utakuwa daraja la kwanza,,,utawashirikisha watu wanne ambao watakuchangia Tshs.1,000 kila mmoja sawa na elfu4,000
[emoji269]utapanda daraja la 2 kwa kuchangia Tshs.3,000 hivyo utabakiwa na faida ya sh.1,000 daraja la kwanza!

✍Daraja la 2: utachangiwa na watu kumi na sita walioletwa na wanne wako kila mmoja Tsh.3,000 (3,000 x 16 =48,000)
[emoji269]panda daraja la 3 kwa kuchangia Tsh.30,000 hivo utabakiwa na faida ya Tshs.18,000 katika daraja la 2.

✍Daraja la 3: utachangiwa na watu 64 Tshs 30,000 kila mmoja sawa na 1,920,000. Hapo utakuwa na faida ya milioni moja laki tisa ishirini elfu.


*MCHANGANUO WA MICHANGO PHASE 2*

Ili kuingia phase ya 2 ni lazima uwe umemaliza phase ya 1. Mfumo huu upo tofauti na mifumo migine, wale waliokuchangia phase ya 1 ndio watakuchangia tena kwenye phase ya 2.

Daraja la 4: utachangiwa na watu 4 uliowaingiza phase 1, kila mmoja Tsh.92,000 (920,000 x 4 = 3,680,000)
[emoji269]panda daraja la 5 kwa kuchangia Tsh.1,500,000 hivo utabakiwa na faida ya Tshs.2,180,000 katika daraja la 4.

✍Daraja la 5: utachangiwa na watu 16 Tshs 1,500,000 kila mmoja sawa na 24,000,000. Hapo utakuwa na faida ya milioni 22,500,000.

Daraja la 6: utachangiwa na watu 64 Tshs 2,000,000 kila mmoja sawa na 128,000,000,000.

CONTACTS
TIGO. 0713216191
VODA. 0767216191 Stan shirima
[11/3, 18:27] [emoji383][emoji387]Administrator[emoji385][emoji383]: Follow this link to join my WhatsApp group: WEKEZA KWA 1000
 
Watu sahv wamehamia kwenye one coin

OVA
 
Back
Top Bottom