Natasha Ismail
JF-Expert Member
- Jul 14, 2008
- 748
- 650
Ni wa bongo fleva au bongo movie?.inasemekana kampuni imeuzwa kwa wasanii wa kitanzania .
Wapendwa,
Nimepata taarifa toka kwa mdogo wangu aliyepo sasatel kuwa hadi leo hii hawajalipwa mshahara wa mwezi wa saba na ule wa mwezi wa sita walipewa nusu tu.inasemekana kampuni imeuzwa kwa wasanii wa kitanzania ambao hata hawajui jinsi ya kuendesha kampuni.wafanya kazi wanahofia kudhulumiwa haki zao zote.
sasatel ipo kwenye market kitambo ila sales zao zimeshindwa kuhit kabisaa , waje tukaange mihogo huku kwa Alimaua B kwetu kuliko usanii
Ni wa bongo fleva au bongo movie?
Haya ndiyo madhira yanayowakumba wafanyakazi wa kampuni zinazoanzishwa mwishoni mwa mwaka (X-Mas time)Kampuni ya simu za mkononi ya SASATEL iko choka mbaya kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Kwa muda sasa hali ya mambo ndani ya shirika hili si nzuri kiasi cha kufikia kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa mafungu.
Wafanyakazi walilipwa nusu mshahara mwezi wa saba nusu iliyobaki hawajalipwa mpaka sasa. Wafanyakazi wana wasiwasi sana kuwa sasa wanaelekea mwisho wa mwezi wa nanae huku hawajalipwa nusu ya mwezi julai.
Huyu mwekezaji vipi?