What is the reason behind losing customers?
Repoti za TCRA hazitoi reasoning, unaweza ukazidownload site ya TCRA.
Ila kuna stepu nyingi walibugi hawa watu, kwanza technolojia wanayotumia ya simu haiko compatible na tulizozoea hapa Bongo, wanatumia CDMA badala ya GSM madhara yake makubwa simu zote za GSM haziwezi kufanya kazi kwenye network yao, kwa jinsi wabongo tunavyobadili sim card daily hili ni tatizo kubwa sana, mambo ya technolojia tofauti yanawezekana US kwa sababu mtu anasign mkataba wa muda mrefu na kampuni ya simu. Jaribu kutafuta simu ta CDMA bongo hakuna options kabisa. Kwa hiyo mtu hauwezi kuswitch kuamua kutumia Sasatel hata ungependa kujaribu, cost ni kubwa i.e kununua simu mpya + sio convenient.
Pia network wameshindwa kuitanua, coverage ni ndogo sana, bila wateja hakuna cash na bila kutanua network hakuna wateja. Bila cash unashindwa kulipa mishahara.
Naamini offer zao zilikuwa ngumu kuelewa/kufananisha kwa watu wengi, zile za lipa 10,000/= upate dakika 200 na SMS 500 (mfano) mbongo akishaona elfu kumi anaacha kusoma anakimbilia vocha ya 500 hata kama hiyo ya elfu kumi ni bora ukipiga mahesabu, na pengine hana hiyo 10,000 anyway.
Copy/Paste ilikuwa nyingi sana kwenye business plan yao kwa kifupi.
Competition ni kubwa sana watu walishusha bei hadi shiling kama sikosei ili kupata wateja nadhani hata kiasi cha kupata hasara sometimes ila sina uhakika, wao wana wateja teyari na wana hela benki so wanaweza kuzichoma kwa muda mfupi ili wakamate market, wewe unaingia kwenye soko unahitaji hela utashindana vipi na mtu ambaye yuko teyari kuuza kwa hasara au karibia na hasara? Inabidi uje na cash kwenye benki na uwe tayari kuzichoma kwa miaka kadhaa ili ukamate soko.
Kuna malalamiko kuwa internet yao sio nzuri ila sijawahi kutumia personally.