Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Cane Growers wakionyesha maboksi ya pedi za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kilombero Sugar leo wilayani Kilombero. Mchango huu, ambao ni sehemu ya mpango wa 'Kukomesha changamoto ya hedhi salama, unaonyesha dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kupambana na changamoto hiyo na kusaidia jamii wanazo zihudumia.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Abraham Mwaikwila (wa pili kushoto), akiungana na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Kampuni ya Sukari Kilombero Bi. Diana Mwakitange (wa tatu kulia), kukabidhi taulo za kike 2,400 kwa Shule ya Sekondari ya Cane Growers iliyopo wilayani Kilombero leo. Mpango huu unaonesha dhamira ya kampuni hiyo katika kupambana na changamoto za hedhi salama na kusaidia jamii ambazo wanafanya kazi. Wengine katika picha ni: - Meneja Mawasiliano na Uhusiano na Wadau, Bw. Victor Byemelwa (wa pili kulia), Meneja wa Masuala ya Biashara, Willa Haonga (kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Cane Growers, Bw. Yusufu Lauwo (kushoto).
Kilombero-Morogoro - Katika jitihada kubwa za kuboresha elimu ya wasichana na kuongeza uelewa kuhusu hedhi salama, Kampuni ya Sukari Kilombero imetoa zaidi ya taulo za kike 2,400 kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Cane Growers iliyopo wilayani Kilombero.
Jitihada hii inaonyesha ahadi ya Kampuni hiyo katika kukabiliana na tatizo la hedhi salama na kusaidia jamii inazo hudumia.
Kupitia hafla ya kukabidhi msaada huo ambayo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Cane Growers, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Ndugu Abraham Mwaikwila, aliipongeza Kampuni ya Sukari Kilombero kwa jitihada zake katika kusaidia elimu ya wasichana. Alisema, "Mchango huu kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero ni zaidi ya msaada bali ni ishara kubwa ya kuunga mkono wasichana hawa wanaosoma ndani ya wilaya yetu. Kwa kutoa taulo hizi za kike, Kilombero Sugar inasaidia kuondoa kikwazo kikubwa kwa elimu. Jitihada hii siyo tu inawasaidia wasichana kubaki shuleni bali pia inawawezesha kuwa na ujasiri wa kufuata ndoto zao bila shida yoyote. Tunashukuru sana kwa mchango huu wenye msaada mkubwa kwa mustakabali wa jamii yetu."
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kilombero Sugar, Bi. Diana Mwakitange, alisema kuwa Kampuni ya Sukari Kilombero leo inakabidhi taulo za kike 2,400 kwa shule kama sehemu ya ahadi yetu ya kibiashara ya kuimarisha jamii tunayoihudumia. Bi. Mwakitange aliongeza kuwa anafurahi kwamba asilimia 65 ya wanafunzi katika shule hii ni wasichana, akisisitiza lengo la kuwahifadhi wasichana shuleni kwa kupambana na tatizo la hedhi salama. Pia alibainisha kuwa jitihada hii inaendana na ajenda ya kitaifa ya kuboresha elimu ya wasichana na kupunguza tofauti za kijinsia shuleni. "Kwa kuhakikisha kuwa wasichana wanapata taulo za kike, tunachangia moja kwa moja katika mafanikio yao ya kitaaluma na ustawi wao."
Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano ya Wadau wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Bw. Victor Byemelwa, alisisitiza dhamira ya Kampuni hiyo ya kuhakikisha hakuna msichana anayekosa shule kwa sababu ya mzunguko wake wa hedhi. "Tunatambua changamoto ambazo wasichana wengi wanakutana nazo katika kusimamia hedhi salama hasa katika jamii ambazo hazihudumiwi ipasavyo. Kupitia shughuli zetu za kurudisha kwa jamii kama hii, tunalenga kuwawezesha wasichana hawa kwa kuwapatia rasilimali muhimu za kusimamia hedhi salama. Kwetu hii siyo tu kutoa msaada wa taulo za kike, bali kuunda mazingira ambapo suala la hedhi salama linakuwa ni la kawaida bila unyanyapaa," alisema Bw. Byemelwa.
Kampuni ya Sukari Kilombero inaendelea kuonyesha dhamira yake ya uwajibikaji wa kijamii kupitia mipango inayoelekezwa kwenye elimu, afya, na maendeleo ya jamii kote Tanzania.
MWISHO
Kuhusu Kampuni ya Sukari Kilombero (KSCL)
Kampuni ya Sukari Kilombero Limited (KSCL), ni mzalishaji mkubwa wa Sukari nchini chini ya chapa maarufu ya "Bwana Sukari". KSCL ni sehemu ya Illovo Sugar Africa Group, mtengenezaji mkubwa zaidi wa Sukari barani Afrika ambaye anajishughulisha na shughuli za kilimo na viwanda katika nchi sita za Afrika; zikiwemo;- Afrika Kusini, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia na Tanzania. Illovo Sugar Africa ni kampuni tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Associated British Foods plc (ABF), iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London. KSCL ipo Kidatu ndani ya Bonde la Kilombero, Kampuni inaendesha mashamba mawili ya kilimo na viwanda vya Sukari; Msolwa na Ruembe vilivyoko katika wilaya za Kilombero na Kilosa na kutenganishwa na Mto Mkuu wa Ruaha, ndani ya Mkoa wa Morogoro. KSCL ina shamba kubwa zaidi la miwa nchini Tanzania lenye ukubwa wa hekta 26,000; hekta 10,000 zinamilikiwa na KSCL na takribani hekta 16,000 kutoka kwa wakulima wadogo maarufu ‘Kilombero Growers’. Kampuni kwa sasa inazalisha tani 126,000 za Sukari kwa mwaka. Mnyororo wa ugavi wa kampuni unajumuisha wakulima takriban 8,000 wakizalisha takriban tani 600,000 za miwa kila mwaka. Asilimia 45 ya miwa inayochakatwa na KSCL inatolewa na wakulima huru; asilimia 55 iliyobaki inatoka kwenye ardhi inayomilikiwa na Kampuni. Zaidi ya biashara 200 zimeanzishwa katika bonde la Kilombero kutokana na mnyororo huu wa ugavi.
KWA MASWALI YA VYOMBO VYA HABARI
Wasiliana na:-Victor A. Byemelwa
Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano ya Wadau
Kampuni ya Sukari Kilombero
Barua pepe: Vbyemelwa@illovo.co.tz