Kampuni ya Tahmeed yaleta mabasi mfano wa ndege

Sisi tulizoea siti mbanano tukivizia watoto wazuri tuanze kutongoza hizo basi hazitufai, sio user friendly kwa kweli
We jamaa nakuunga mkono na miguu kwa kweli watatuharibia sana kwa staili hii
 
Tangazo limekosa logo tu.
Kuna RATCO, KIMBINYIKO, TABORA EXPRESS, SHABIBY, BUTI LA ZUNGU wote hao wanazo
Nimewahi kupanda RATCO Dar to Tanga, na Buti La Zungu Dar to Mtwara. Lakini tofauti ipo. Kwanza mengi ya hayo magari yana portion tu ambayo ni executive hasa mbele na huwa kuna separation. Kipekee haya yapo classic.
Hujatuambia ni route gani watapelekewa. Lakini nafikiri ni Arusha, Tanga/Mombasa,Dodoma,Iringa,na Mtwara. Hizo route siyo za umbali wa kutisha sana, kakini abiria wake hupenda mabasi ya kisasa.
 
Mbona kuna kampuni ya shabiby na Tabora One zina mabasi hayo toka dar tabora na dar dom kila siku toka 2015! Jitahidi kufanya tafiti kabla ya kuandika, usije andika utumbo broh.

Ati yanafanana na ndege aina ya Boeing, seat configuration ya Boeing ni 1 X 2? kweli?

Kaja na povu nahisi anapakiwa bure ili apigie debe
 
Tahmeed is a Kenyan company sielewi kwa nini wanapewa ruhusa kuserve domestic routes. Serikali amkeni!
 
Declare interest...koz kila ukija unakuja na post za tahmeed tu..ukiponda mabasi mengine mathalan klm...weka wazi tu wewe ni mwajiriwa au ndugu au chochote kinachokuhusisha na tahmeed...koz ujio wa basi mpya ni inside info...then muwe mnalipia matangazo!
 
Hongera haya ndo mambo tunataka kuyaona, ushindani kwa ubora na huduma.... Wengine watajifunza kwenu na watakuja na za airbus na zingine ....
 
Braza vipi wapiga gear tunaruhusiwa kutuma maombi uzoefu miaka 31 barabarani!
 

Mwendokasi pia 2 by 1
 
Ni mazuri ila siti za kati watakuwa wanasumbua sana watu wa dirishani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…