Kampuni ya Total ya Ufaransa yashutumiwa kwa kusambaza mafuta ya ndege kwa jeshi la Urusi

Kampuni ya Total ya Ufaransa yashutumiwa kwa kusambaza mafuta ya ndege kwa jeshi la Urusi

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Waziri wa Uchukuzi wa Ufaransa alitoa wito wa kuangazia mazingira ya kashfa hiyo inayozunguka tuhuma za kampuni ya mafuta ya TotalEnergies kuisambazia Urusi mafuta kwa mahitaji ya jeshi la anga la Urusi.

Tofauti na makampuni mengi makubwa ya Magharibi ambayo yameanza kufanya biashara nchini Urusi, TotalEnergies bado inamiliki karibu nusu ya hisa katika uwanja wa gesi ulioko nchini Urusi.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinadai kuwa gesi inayozalishwa huko hutumika kuzalisha mafuta ya ndege, ambayo hutumiwa na ndege za kivita za Urusi nchini Ukraine.

Usimamizi wa TotalEnergies ulipuuzilia mbali madai haya na kusema kuwa hayana msingi.

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi wa Ufaransa Clement Bon aliingilia kati.

“Hii ni mada nzito sana,” alisema kwenye kituo cha TV cha France 2.

“Kwa hivyo, ni muhimu kujua kama kumekuwepo - sio muhimu sana iwe ni kwa makusudi au la - ukiukaji wa sheria ya vikwazo au matumizi mabaya ya nishati inayozalishwa na kampuni yoyote – ya Ufaransa au nyingine yoyote’’.

================

Mnarukaruka weee ila kiukweli ulaya haiwezi kuishi bila Russia na Ukraine na ndio maana Putin anataka kukamata rasilimali za Ukraine ambazo zinaweza kuipa ahueni Ulaya ambazo hapo awali zilikuwa chini ya Soviet

Mtaisoma namba this time KGB kakalia usukani
 

Attachments

  • Screenshot_20220826-101332_Facebook.jpg
    Screenshot_20220826-101332_Facebook.jpg
    203.6 KB · Views: 8
Back
Top Bottom