KERO Kampuni ya ulinzi WS Insight iliyopo Masaki, acheni kuwatesa wafanyakazi wenu

KERO Kampuni ya ulinzi WS Insight iliyopo Masaki, acheni kuwatesa wafanyakazi wenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Garnacho

Member
Joined
Jan 11, 2023
Posts
23
Reaction score
34
Kampuni hii imekuwa na kawaida ya kuwalipa wafanyakazi wake (Walinzi) kwa kucheleweshewa mishahara, mfano mwezi uliopita walilipwa tarehe 11/07/2026 huku kwa mwezi huu wa nane kukiwa hakuna hata mmoja aliyelipwa mpaka sasa.

Tunaomba wizara husika kuifatilia kampuni hii kwa kina, kwani imekuwa ikiwatesa wafanyakazi wake ambao hawana wa kuwatetea

Jambo lingine kuhusu kampuni hii ni kutoongezwa mishahara kama serikali ilivyoagiza mwaka jana kuwepo kwa ongezeko la mishahara kwa private sectors, ila kwa kampuni hii hilo halikufanyika na wafanyakazi hawajui wakadai wapi haki yao.

Waziri husika fatilia jambo hili, WAFANYAKAZI WA HII KAMPUNI WANATESEKA! 🙏
 
Back
Top Bottom