Kampuni ya Umeme yaikatia huduma Ofisi ya Halmashauri, nayo yamwagiwa Uchafu mlangoni kwa kudaiwa kodi na Halmashauri

Kampuni ya Umeme yaikatia huduma Ofisi ya Halmashauri, nayo yamwagiwa Uchafu mlangoni kwa kudaiwa kodi na Halmashauri

Tuache na taasisi zetu kwani zimetajwa wapi kwenye hii thread kwani wangewekeana makubaliano ya kulipana kwa awamu kiustarabu na kwa staha kingeharibika au ni kukosa tu maarifa ,uongozi ni jalala na pia ni jaala ya maulaana sio kudandia tu .
Na HEKIMA wale watu hawana HEKIMA kabisa
 
Kipaumbele chao kilikuwa katiba mpya.Inafanya kazi vizuri.Just imagine ingetokea Tanzania wavimba macho wangekuwa na a field day.
Yaani wewe unaona kweli Katiba Mpya inafanya kazi vizuri kwa ujinga huo!!?
 
Yaani wewe unaona kweli Katiba Mpya inafanya kazi vizuri kwa ujinga huo!!?
Kwani mwisho wa matatizo ya Nchi yeyote sio katiba mpya?Au nimeelewa vibaya.Wavimba macho si walikuwa wanawasifia sana Kenya kwamba wana katiba mpya?Hivyo matatizo yote yatakwisha?
 
Ila wakenya asee 😀😀😀, na hapo wamezuia matumizi ya mpepe, hawa watu si bure waliunda mungiki wana kaujasiri fulani kakifala 😁😁
 
Kwani mwisho wa matatizo ya Nchi yeyote sio katiba mpya?Au nimeelewa vibaya.Wavimba macho si walikuwa wanawasifia sana Kenya kwamba wana katiba mpya?Hivyo matatizo yote yatakwisha?
Hebu onyesha mahusiano ya Katiba Mpya na hicho kilichotokea. Kwenye Katiba ya Kenya kumeandikwa kuwa taasisi ikidaiwa fedha isilipe bali imwage uchafu kwa wadai wake!?
 
Kwani mwisho wa matatizo ya Nchi yeyote sio katiba mpya?Au nimeelewa vibaya.Wavimba macho si walikuwa wanawasifia sana Kenya kwamba wana katiba mpya?Hivyo matatizo yote yatakwisha?
Yaani watu wa CCM uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Katiba Mpya na kwisha Kwa matatizo kunahusianaje?
 
Nashangaa unashangaa kwamba Katiba Mpya ndio huwa mnaiimba kwamba ndio suluhisho la matatizo yote.Linapotokea tatizo huwa hamtafiti kwanini limetokea kwenye uwajibikaji bali huwa mnasema tunahitaji katiba mpya.
At least now umeanza kujua kwamba katiba mpya sio suluhisho la kila kitu.
Niliandika kama sarcasm.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Imenikumbusha ile vita ya kitambo ya Tanesco na Dawasco.. waliwakatia umeme na na wao wakawakatia Maji mbwai mbwai tu...

And ile mbungi ya Polisi waliokuwa wakipita njia ya Mwendo kasi wakakutana na maaskari wa njia ya mwendokasi wakawekewa misumali wasipiite mziki ukawa poa sana.
 
Hii inaitwa ubaya ubwela

Mwosha. Huoshwa

Yaani

Kampuni ya umeme Kenya inadai HALMASHAURI WAKAKATA UMEME

Nao WANADAIWA KODI na HALMASHAURI mashallah wakamwaga UCHAFU MLANGONI

Hii n ubaya ubwelaa

=====

Halmashauri ya Jiji la Nairobi yaziba njia ya maji taka katika ofisi za Kenya Power & Lighting (KPLC) katikati ya jiji la Nairobi, hali iliyopelekea kumwagika na kutiririka kwa majitaka ghafi huku mvutano kati ya KPLC na City Hall ukiendelea.

Mapema leo, Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) iliagiza City Hall kuondoa taka zote zilizoachwa katika Stima Plaza siku ya Jumatatu, ikieleza kuwa kitendo hicho ni cha kizembe na kinaweza kuhatarisha mazingira.

KPLC inailaumu serikali ya Kaunti ya Nairobi kwa kushindwa kulipa deni lake la umeme linalofikia KSh bilioni 3, huku kaunti nayo ikidai KPLC ina deni la KSh bilioni 4.8 kutokana na ada za njia za umeme (wayleave fees), hali inayosababisha mvutano mkali.
View attachment 3250063

Source: BuzzroomKenya
Wakenya,wanatakiwa wake huku kwetu watupe mafunzo na ujasiri.
Tunateseka sana
 
Back
Top Bottom