Kampuni yasimamishwa kununua majani ya chai

Kampuni yasimamishwa kununua majani ya chai

BabuK

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2008
Posts
1,845
Reaction score
329
kiwanda-chai_210_120.jpg


KAMPUNI ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imepigwa marufuku kuendelea kununua majani ya chai kutoka kwa wakulima wa zao hilo mkoani Mbeya na badala yake kiwanda chake kitumie majani yaliyopo kwenye shamba walilobinafsishiwa na serikali.

Kwa muda mrefu, MeTL kupitia kiwanda chake kilichopo wilayani Rungwe, imekuwa ikikiuka taratibu za leseni yake kwa kununua majani kutoka kwa wakulima wadogo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku ununuzi huo aliodai unakwenda kinyume cha leseni yao ambayo inawataka kutumia majani yaliyopo kwenye mashamba yao pekee kutokana na kujiingiza huko, kumekuwapo na mgongano mkubwa kwa wakulima, hatua inayosababisha kuwepo na makundi yanayolumbana.

Alisema pia Kiwanda cha Chai cha Kampuni ya Wakulima Tea Company (Watco) kilichopo Katumba wilayani hapa, ambacho kimsingi ndicho chenye mamlaka ya kununua chai ya wakulima, kimekuwa na wakati mgumu kwa kutopata majani yanayotosheleza kwa ajili ya uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Busokelo, Eston Ngilangwa alisema, amekuwa akiwaona MeTL wakinunua chai kwenye eneo lake pasipo kupewa kibali na halmashauri na akasema mkakati uliopo ni halmashauri kulenga kumchukulia hatua kwa ukaidi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Ezekiel Mwakota alisema mpasuko uliopo ndani ya wakulima wa chai wilayani hapa umesababisha hata zao hilo kukosa ubora unaotakiwa kwa kuwa kila mnunuzi amekuwa akijiwekeza viwango vyake.

Ofisa Kilimo na Huduma za Ugani wa Kiwanda cha MeTL, Hashim Ibrahim alisema, kampuni hiyo ilianza kununua chai ya wakulima baada ya wakulima wenyewe kuomba chai yao inuniliwe hapo badala ya Watco waliyosema inawanyonya kutokana na bei ndogo.

Chanzo: HabariLeo
 
Maslahi ya kibiashara..kuna rafu nyingi sana huchezwa kupata kile unachohitaji ili kutimiza malengo yako
 
Back
Top Bottom