MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Kwa muda mrefu sasa, kampuni za kibiashara zimekuwa zikichangia katika miradi ya kijamii. Uchangiaji huu umechagizwa kwa kiasi kikubwa na hoja ya kwamba "Jamii yenye afya na ustawi mzuri (healthier community), huchochea ukuaji wa biashara". Mwaka 1936 nchini Marekani kiasi cha Shilingi Biliono 69 kilitolewa na kampuni za kibiashara kwa ajili ya Miradi ya Kijamii, mwaka 2008, kiasi kilipanda mpaka kufikia Shiilingi Trilioni 32.
Peter F. Drucker anaamini kwamba kampuni za Kibiashara zinapaswa kutoa/kuchangia kiasi cha faida zao kwa jamii kutokana na sababu kuu mbili;
- Shughuli za kampuni kwa namna moja au nyingine zinaweza kuwa na madhara kwa jamii husika, mfano kampuni za uchimbaji wa madini na uharibifu wa mazingira, viwanda na utoaji wa hewa chafu. Hivyo kwa madhara haya ni wajibu wa kampuni kuchagia maendeleo ya jamii (kama fidia)
- Kampuni "as a corporate citizen" kwa namna yoyote lazima iguswe na matatizo ya jamii, kwa mfano; huwezi ukaanzisha kiwanda kwenye jamii ambayo ina matatizo ya lukuki ya kiafya, kwa sababu matatizo ya kiafya (i) yatakukosesha nguvu kazi (ii) yatawafanya waathirika wa matatizo hayo washindwe kuzalisha na kukosa kipato cha kuwawezesha kununua bidhaa/huduma zako. Kwa muktadha huu, kampuni lazima ishughulike na matatizo ya Kijamii ili iweze kuchanua katika biashara zake.
- Utoaji wa fedha
- Utoaji wa bidhaa , kwa mfano utowaji wa vinywaji kwa washiriki wa Mradi (endapo umeifuata kampuni ya vinywaji kwa ajili ya kuchangia mradi)
- Utoaji wa wafanyakazi kwa ajili ya kujitolea/kutoa maarifa kwenye Taasisi/kwenye utekelezaji wa Mradi wako
- Michango ya wafanyakazi (matching gift for employees).Kuna baadhi ya kampuni zimeweka utaratibu wa kila mfanyakazi kukatwa kiasi fulani cha fedha kila anapopokea mshahara, na kiasi hiki hutolewa kwa ajili ya kusaidia jamiii
Unapozijumuisha kampuni za kibiashara katika utekelezaji wa mpango wako wa harambee (Fundraising Strategy), ni muhimu kufahamu mitindo inayoongoza kampuni za kibiashara katika utoaji kwa jamii, uelewa wa mitindo hii, itakusaidia kujua namna nzuri na sahihi ya kuzifuata kampuni hizo kwa ajili ya mradi wako. Mitindo hii, ni kama ifuatavyo;
- Corporate Productivity Model: "Model" hii imejengwa na dhana (premise) kwamba, utoaji wa kampuni kwa jamii hupelekea mauzo ya kampuni kuwa juu na hatimae kampuni kupata faida. Hivyo basi kwa muktadha wa "model" hii, kampuni itakuwa tayari kuchangia miradi ambayo (i) itatangaza bidhaa/huduma za kampuni (ii) itajenga taswira nzuri ya kampuni kwenye jamii n.k
- Stakeholder Model: "Mode" hii imejengwa na dhana (premise) kwamba kampuni ina jukumu la kukidhi haja na matamanio ya makundi mbalimbali ya wadau (stakeholders), makundi haya hujumuisha wafanyakazi (employees), wanahisa (shareholders), wateja (customers), wazabuni (suppliers) serikali (government agencies) n.k. Hivyo basi kwa muktadha wa "model" hii, kampuni itakuwa tayari kuchangia miradi ambayo itagusa maslahi ya wadau wengi, mfano miradi ya elimu, miradi ya mazingira n.k
- Ethical Model: "Model" hii imejenga na dhana (premise) kwamba; kampuni pamoja na viongozi wake wana wajibu wa kuwa wananchi bora kwenye jamii, hivyo wanapaswa kujitolea kuisaidia jamii (Corporate Social Responsibility). Hivyo basi kwa muktadha wa "model" hii, kampuni itakuwa tayari kuchangia miradi ambayo; itajikita kwenye matatizo ya msingi ya jamii, hususani maeneo ambayo kampuni inaendesha shughuli zake.
- Political Model: "Model" hii imejengwa na dhana (premise) kwamba; ili kampuni iwe na nguvu, kinga na ushawishi kwenye jamii na mamlaka, haina budi iwe na utaratibu wa kuchangia jamii. Miradi ya mazingira, Miradi ya udumishaji wa amani ni muafaka kwa kampuni zinazoamini "model" hii.
AHSANTE
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising &Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA