Kampuni za kigeni zina nafasi gani katika kufanya biashara Tanzania?

Kampuni za kigeni zina nafasi gani katika kufanya biashara Tanzania?

wanzagitalewa

Senior Member
Joined
Jan 25, 2018
Posts
128
Reaction score
84
Katika siku za hizi karibuni naonekana ni vigumu sana kwa wiki moja kupita bila kuwapo taasisi yoyote itakayochapisha ripoti kuhusuTanzania. Wiki iliyopita ilikuwa zamu ya Benki ya Maendeleoya Afrika (AfDB).

Katika chapisho lao kuhusu muonekano wa uchumi waTanzania kwa mwaka mmoja, walituambia jambo ambalo tayari limekuwa linasemwa mara nyingi nchini; kwamba uchumi wetu unakua. Aidha, AfDB wametabiri kuwa, kwa mwaka 2018, uchumi wa Tanzania utakua kwa 6.7%. Hii ni habari nzuri.

Lakini ndugu zetu wa AfDB wametoa tahadhari moja kwetu; ni tahadhari ambayo nadhani inatupasa kuichukua kwa umakini mkubwa. AfDB walisema, kutokutabirika kwa mazingira ya biashara, kunaweza kuwaondoa wawekezaji katika sekta binafsi.

Wanamaanisha nini? Wanaamini kwamba, wawekezaji hasa kutoka ughaibuni wanaokuja kuwekeza Tanzania wana wasiwasi kuhusu masuala ya sera, sheria na rushwa nchini. Natukubali kwamba, AfDB kusema hili, tusichukulie kama ni jambo dogo kwani wanaheshima kubwa katika masuala ya uchumi, hata wakati mwingine tunakopa kwao au tunategemea watudhamini kwa kauli njema ili tuweze kupata mikopo sehemu nyingine.

Kwanini ni wa muhimu? Kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa 6.7% tunachozungumzia, kinategemea kwa kiasi kikubwa uwekezaji kutoka nje ya nchi. Ukuaji wa uchumi wetu unaendeshwa na kampuni za nje ambazo zimewekeza nchini na kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za kibenki na mawasiliano.

Mfano, Watanzania zaidi ya 70% wanaoishi vijijini, hupata huduma ya fedha kupitia mitandao ya simu, ni hii ni muhimu sana kwao. Makampuni ya kimataifa yanaleta fikra mbadala na namna mpya ya kufanya biashara hapa nchini. Kampuni hizi zinawasaidia watu kufikia malengo yao kutokana na huduma na bidhaa wanazotoa.

Kwa kiasi fulani, ukweli huu utakuwa unauma. Tukumbuke kuwa makampuni ya nje yanaleta faida nyingine kupitia mapato ya kodi na kupandisha kiwango cha maisha cha wananchi wa Tanzania. Hayumkini, wewe unayesoma makala hii sasa hivi unafanya kazi kwenye kampuni ya kigeni kwa namna moja au nyingine.

Hiki ni kitu ambacho majirani zetu wa Rwanda wamekigundua na sasa wamekumbatia soko huria na wawekezaji wanazidi kwenda nchini humo. Nchini Kenya, kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji ni moja ya vipaumbele vyao vya kwanza, japo kwa kiasi kikubwa siasa za nchi hiyo zinakwamisha hilo.

Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya kufanya biashara. Kama hawatarekebisha kasoro zilizopo, wawekezaji wa kimataifa hawawezi kuleta miradi mikubwa nchini.

Jambo kubwa zaidi ni kuwa, mbali na kurekebisha mazingira ya kibiashara, serikali iendelee na moto wake wa kuwachukulia hatua kali wale wote wanaojihusishana vitendo vya rushwa.

Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa mkali katika hili. Anafahamu kuwa rushwa ni lazima itokomezwa. Lakini pia atengeneza mazingira imara kwa ajili ya sekta binafsi kufanyabiashara. Linapokuja suala la kufanya biashara ili tupate faida katika dunia hii ya ushindani, tunatakiwa kuifanya Tanzania kuwa namba moja kuvutia wawekezaji, maana yake kuushinda huo ushindani sokoni na kupata faida kwa Taifa letu.

Wanzagi Talewa Nyaronyo

Musoma, Mara

wanzagi.talewa@gmail.com
 
Back
Top Bottom