Kampuni za simu kuongeza bei kiholela ni kuidharau Serikali au kuna ubia na Viongozi?

Kampuni za simu kuongeza bei kiholela ni kuidharau Serikali au kuna ubia na Viongozi?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Hakika hii sasa ni kero ambayo inaonesha Serikali ya CCM imeshindwa KABISA kusimamia kampuni za biashara hususani za Simu na yanafanya chochote watakacho na hakuna cha kuwafanya.

Nimeshtuka asubuhi hii kukuta wameongeza tena gharama za vifurishi na kwa speed hii hadi kufikia December tusishangae shs 1,500/ tukajikuta inanunua MB 100 tuu huku viongozi wa Serikali ya CCM wao wakiendelea kugonga glass za mvinyo huko Serena

Screenshot_20220729-074106_Phone.jpg
 
Tatizo lilianza kwa sisi wananchi kulalamika, serikali ikatusikiliza ikawatungia bei kikomo, hapo ndo shida ilipoanza
 
Mbaya zaidi hao wahusika wakusimamia na wenyewe wanatumia vifurushi hivyohivyo wanaona mabadiliko na wamenyamaza kama wao hawasemi nani atasema Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote😍
 
Tuwapigeni sanctions za kususia mitandao yao, hadi washushe bei. Hatuwezi kuwawajibisha ilhali tunaendelea kwa mtindo huu kujaza bando zao kila baada ya dakika ^tar-know!^
 
😂😂😂😂😂😂😂

Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa... Nyie ambao kila siku mnadai mambo yako sawasawa kumbe hata hamjui maisha wanaoishi wavuja jasho wa Tanzania yakoje!!??
Hapa Tigo GB 1 ni tsh 2000

Ndio sababu nimemuuliza bwashee!
 
Yani nimeshtuka Leo Kuna kifurushi Cha halotel nilikuwa napata dk80 na gb1, Leo napata dk 30. So sad
 
Back
Top Bottom