Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Kuna kitu inabidi tujiulize kuhusu makampuni ya simu na huduma tunazostahili kupata kutoka kwao, huduma ambazo ni haki yetu kupata na wala hatupewi msaada. Shida inatokea pale watanzania wapoona makampuni haya ya simu yanatuhurumia kutupatia huduma hizi na kwamba bila ya huruma yao basi huduma hizo sizinge tolewa kwetu. Unalipia huduma hizo hivyo ni haki yako kupata kila unachostahili kutoka kwao na sio mpaka wajiskia kuzitoa!
Je, sisi kama watumiaji wa mitandao ya simu kutoka kampuni mbalimbali nchini tunajua ni nini makampuni haya wanapaswa kutupatia? Tunajua thamani ya data tunazopewa kama zinaendana na thamani ya pesa tunayolipia? Yaani mfano kwa Sh. 10,000 upewe GB 5 za data, je una uhakika kweli kwa pesa hiyo unapatiwa Gb 5 kweli?
Vipi kama unapewa pungufu, kwenye simu yako kweli ujumbe unasoma GB 5 lakini kiuhalisia umepewa GB 2? Kuna njia gani ya kuweza kujua ukweli wa mambo kwenye makampuni haya ya simu? Au mpaka tukubaliane kwa umoja wetu kususia kampuni mojawapo ya simu kwa wiki moja tu ndio waanze kuwajibika katika huduma zao?!