Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Kuna kitu inabidi tujiulize kuhusu makampuni ya simu na huduma tunazostahili kupata kutoka kwao, huduma ambazo ni haki yetu kupata na wala hatupewi msaada. Shida inatokea pale watanzania wapoona makampuni haya ya simu yanatuhurumia kutupatia huduma hizi na kwamba bila ya huruma yao basi huduma hizo sizinge tolewa kwetu. Unalipia huduma hizo hivyo ni haki yako kupata kila unachostahili kutoka kwao na sio mpaka wajiskia kuzitoa!

Je, sisi kama watumiaji wa mitandao ya simu kutoka kampuni mbalimbali nchini tunajua ni nini makampuni haya wanapaswa kutupatia? Tunajua thamani ya data tunazopewa kama zinaendana na thamani ya pesa tunayolipia? Yaani mfano kwa Sh. 10,000 upewe GB 5 za data, je una uhakika kweli kwa pesa hiyo unapatiwa Gb 5 kweli?

Vipi kama unapewa pungufu, kwenye simu yako kweli ujumbe unasoma GB 5 lakini kiuhalisia umepewa GB 2? Kuna njia gani ya kuweza kujua ukweli wa mambo kwenye makampuni haya ya simu? Au mpaka tukubaliane kwa umoja wetu kususia kampuni mojawapo ya simu kwa wiki moja tu ndio waanze kuwajibika katika huduma zao?!​
 
Kuna App za kutrack matumizi yako ya data kwa siku.

Pia unaweza ukacheki by default kwenye cm yako ukareset data usage ikasoma 0kb hafu ukaanza kuona jinsi App zinavyotumiq datq na total iwe iyo 10GB.

Mfano kwenye iPhone:

Hapo current period 64GB kuna mahala ukireset inasoma 0 hafu unaanza kutumia sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…