Kampuni za simu, uhakiki taarifa za mteja usiishie kwenye jina na muamala wa mwisho pekee, wateja wanalizwa huku

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu, kuna text niliona inasambazwa huko duniani, jinsi wezi wanavoweza kuhamisha pesa kutoka kutoka Mpesa, TiGO pesa, na walet nyingine.

Ukiibiwa simu ukiwa hauitumii ndani ya muda huo (yaani iko locked) utakuwa na muda kidogo kabla kaka jambazi hajafanya lake.

Ukiibiwa simu ikiwa unaitumia (yaani haiko locked) hapa ndio kuna balaa na wengi wamepigwa kwa njia hii.

Kaka jambazi atapiga #106# kuangalia usajili wa line hiyo, hapo litatokea jina kamili la aliyeibiwa simu pamoja na namba yake kamili. Kaka jambazi akimaliza hapo atatuma pesa kwenye namba hiyo kama buku au 500, ambapo pesa ikipokelewa muamala utasoma kiasi alichotumiwa pamoja na salio kamili lililopo kwenye simu(kama simu ilikuwa na hela).

Hapo sasa kama una hela nyingi, tayari kaka jambazi ana muamala wa mwisho (ikiwa aliyeibiwa simu ni mtu wa kufuta sana msg na hakuna rekodi kwenye simu yake) na pia ana jina kamili la mhusika. Sasa hapo ni ama ajifanye amekosea namba ya siri mpaka simu awe locked kwenye huduma ya Mpesa/Tigo Pesa au yoyote iliyotumika au apige moja kwa moja huduma kwa wateja na kusema amesahau namba yake ya siri.

Mtoa huduma atamuuliza jina lake kamili pamoja na muamala wa mwisho kufanyika kwenye simu yake, mtoa huduma akishapewa taarifa hizo zote, kaka jambazi anatumiwa namba ya siri mpya kama muhusika na mchezo unakuwa umeisha hivyo. Umeibiwa simu na pesa juu.

Watoa huduma wa simu, mtu akipiga simu kubadili namba yake ya simu maswali yasiishie tu kwenye muamala uliopita pamoja na jina la mtu maana kama mtu si wa kufuta msg jumbe zote za miamala ni rahisi tu.

Walau maswali yazidi kwenye namba ya kitambulisho. Na wewe unayeibiwa simu changamka ukishaibiwa chaap uwahi kufunga line yako kabla ya kitu chochote, maana unaweza usiwe na hela kwenye simu yako lakini namba yako ikatumika kufanyia utapeli na worse ikahusika kwenye uhalifu mkubwa au hata mauaji, mpaka uje uthibitishe sio wewe bali uliibiwa simu utakuwa umeshahaia na kupoteza vingi.

Tuwe makini jamani.
 
Pia huwa wanauliza tarehe, mwezi na nwaka wa kuzaliwa pamoja na majina yako matatu. Kibaka hawezi kuwa na TAARIFA hizo.
 
Kwhyo kibaka atajua adi jina la mama yangu..eeeh
 
Bora wafanye kuwa ukibadilisha PIN tu, account isifanye kazi hadi yapite masaa 24.
 
Sema huduma ya kufungua line zilizojifunga ifanyike kwenye ofisi zao au mawakala ambao wako verified na hiyo mitandao, mambo ya taja tarehe ya kuzaliwa ni ujinga
 
Wameadd swali la kiulinzi kama jina la utani lako au timu ya mpira

mimi nimeweka waniulize sehem gani ya mwili wifi yenu anaipenda Nmesave NDONGA
 
Back
Top Bottom