A
Anonymous
Guest
Mimi ni mmoja wa wananchi tunaotumia huduma za simu za mkopo. Kwa kweli tunakumbana na changamoto kubwa sana kwenye huduma hii.
Mara nyingi wanatukopesha simu ambazo siyo nzuri nyingi zina matatizo. Simu unachukua leo, baada ya siku chache tu inaanza kusumbua. Ukienda pale Milimani CT utakuta watu wengi sana wanarudisha simu zao kwa sababu ya hitilafu mbalimbali.
Cha kusikitisha ni kwamba hata ukirudisha simu kwa ajili ya matengenezo, unaweza kuambiwa uiachie hapo itengenezwe, halafu uchukue baada ya siku tatu au zaidi. Hii inatuathiri sana kwa sababu simu ni kifaa muhimu kwa mawasiliano na shughuli zetu za kila siku.
Licha ya matatizo hayo, gharama wanazotutoza ni kubwa sana. Tunaendelea kulipa pesa nyingi kwa simu ambazo zinaonekana tayari zimetumika au zina ubora wa chini.
Kutokana na hali hii, tunahisi kama kuna udanganyifu au ukosefu wa uwazi katika huduma hii. Tunaomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli na kulinda haki za wateja.
Kwa sasa hali hii inatupa usumbufu mkubwa na tunahitaji msaada wa haraka.”