Kamwe atangaza ratiba ya Wiki ya Wananchi

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kumbe na kwenye soka kiki ni dili!

… Tumewaambia kilele ni August 4, lakini kama ilivyokuwa utamaduni wa Yanga sisi tuna Wiki ya Wananchi ambayo kilele chake ni ndiyo August 4, na hiyo wiki ndiyo inaanza leo (Julai 29, 2024)

Timu itawasili leo saa tisa usiku kutoka Afrika Kusini uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, naomba nichukue nafasi hii kuwaomba mashabiki wa Yanga kote Dar twendeni leo tukawapokee anajeshi wetu na tuwaoneshe kwamba tunaanza kwa kishindo season hii ya 2024/2025.

Pia soma: Tetesi: - Ally Kamwe arudishwa kwenye nafasi yake kama kawaida

Siku ya kesho Jumanne Julai 30, 2024 kutakuwa na tukio kubwa la kumtambulisha mdhamini wetu mkuu wa wiki ya wananchi

Siku ya Jumatano Julai 31, 2024 ni siku ya kufanya usafi, na kwamba hapa Dar eneo ambalo limechaguliwa kufanya usafi ni Hospitali ya Temeke. Lakini hizi ni sherehe za wana Yanga sehemu zote, maana yake kila mkoa, wilaya na mtaa ambako mashabiki wa Yanga wapo wanatakiwa kutenga siku hii kuwa maalum ya kwenda kufanya usafi. Klabu itatangaza kila shughuli ambayo itafanyika kwa kila mkoa

Siku ya Alhamisi Agosti 1, 2024 wana Yanga tutakutana kwenye kuchangisha damu. Siku hii pia itakwenda sambamba na activation kubwa ya hamasa ambayo itafanyika Mbagala Zakhem

Siku ya Ijumaa Agost 2, 2024 ni siku maalum ya kitaifa kuomba dua kwaajili ya wana Yanga na wale tuliokuwa nao ambao wametangulia mbele za haki

Siku ya Jumamosi Agosti 3, 2024 tutaandaa jogging makao makuu ya klabu ambayo itakwenda sambamba na supu

Siku ya Jumapili Agosti 4, 2024 ndio kilele cha Wiki ya Wananchi, pale Uwanja wa Benjamini Mkapa, ambako kutakuwa na mechi siku hiyo

Tabu Iko pale pale
 
Back
Top Bottom