Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,641
Kuna Mzee Mmoja ( Jina Kapuni ) japo alishawahi Kuniongoza Kikatiba huko nyuma taratibu sasa naanza kuona jinsi ambavyo huenda Ugonjwa wa Moyo utakavyoanza Kumuathiri na pengine hata Israeli anaweza Kuamua Kuondoka nae mapema tu kwenda katika Mapumziko yake ya Milele.
Sababu kubwa ni kwamba kama kuna Mzee ambaye si tu alikuwa anajikomba bali bado pia anajikomba kwa Joni huku akijiaminisha kabisa kuwa iwe isiwe Mwanae Mpendwa aliyeyazoea Maisha ya kuishi na Wanajeshi kwa miaka mingi atakuja nae Kuirithi Kazi yake huko kwa Waunguja na Wapemba ila kwa upepo unavyoenda sasa Mwanae huyo hiyo Kazi ataisikia tu katika Bomba.
Si tu kwamba Joni hataki Kuongozana na Hussein katika Safari yake ya kwenda Kisiwani Zanzibar ila anaogopa kuwa huenda huko mbeleni akaja Kumsumbua hasa ukizingatia Hussein kaanza kuwa katika Mfumo kabla yake na ana Mtandao mkubwa ulioratibiwa vyema na Baba yake alipokuwa Kazini hivyo anaona bora tu asafiri na Makame ambaye amemzoea na anammudu vilivyo kabisa.
Na kinachosikitisha na hata kutia Huruma kabisa ni kuwa tayari Hussein alishaanza Kuuvaa uhusika wa hiyo Kazi anayoenda Kuikosa na Kuijutia.