tatizo kubwa ambalo tunalo katika nchi hii ni mifumo ya utawala imeungana. hatuna mihimili mitatu ya utawala kwani katiba zote kwa maana iliyopo na iliyopendekezwa zimeua mihimili hiyo na tumebaki na mhimili mmoja na mihili mingine kuwa kujiunga na .
lengo la kuwa na mihimili mitatu nadhani ni kile wanachoita checks and balance.
lengo hapa la mihimili mitatu ni kuhakikisha katika utendaji iwapo kuna mmoja amejisahau katika hiyo mihili basi hawa wengine wanareact, si kwa ajili ya ubaya bali lengo ni kuhakikisha uongozi hautoki kwenye malengo.
unapokuwa na mahakama ambayo ipo ndani ya wizara ya serikali na mahakama hii inatokana na serikali kwa mfumo ni wazi huwezi kuwa na mahakama iliyo sawa na serikali yenyewe ili kutoa checks and balance iwapo kutatokea tatizo kwa upande wa serikali.
lakini pia unapokuwa na wabunge ambao wamo ndani ya serikali na wabunge wakiteliwa kufanya kazi ndani ya serikali unakuwa na bunge lenye wabunge wanaotafuta nafasi za utumishi serikalini na mijadala na hoja zote zinakuwa ni za kujitengenezea mazingira au kulinda maslahi yao.
hivyo huwezi kupata checks and balance kitu ambacho ni muhimu sana katika utwala wan chi.
Matokeo yake ni kuwa na corrupt au weka judicial system, kuwa na corrupt government na kuwa na weak and hypocrisy parliament.
Haya ndiyo mambo ambayo checks and balansi katika utawala inatakiwa kuondoa.
Lakini kama kuna corruption katika mfumo wa mahakama nani wa kuinitiate mabadiliko?, nani wa kupitisha madiliko? Haya yalikuwa majukumu ya serikali na bunge lakini wameungana na kuwa kitu kimoja hivyo hakuna wa kumfunga paka pengele.
Kama kuna corruption katika government nani wa kusimamia kuona kama kinachotendeka ndicho kilichostahili au kimetoka katika mstari?, nani wa kutoa maamuzi kama yanahitajika kuwa hapa kweli kuna makosa yamefanyika? Haya ni majukumu ya bunge na mahakama.
Iwapo chombo hiki cha wananchi ambacho ndicho chenye mamlaka ya juu kwa kuwa wao ndio wamekasimiwa baadhi ya madaraka ya wananchi hivyo wao ndio wanawakilisha wenye mali. Hawa tunaweza kuwalinganisha na bodi katika kampuni yetu ambayo ni serikali. Lakini hawa wanaweza nao kufanya mambo kama kutoa maamuzi yaliyo nje ya mipaka yao, kujisahau na kutaka kuingilia kazi zisizo kwao hivyo mihimili mingine ambayo ni serikali na mahakama zipo kuweza kuyaweka bayana mambo haya.
Lakini vyombo hivi vinapokuwa vimeungana basi ile dhana ya kuwa na vyombo vitatu inapotea kabisa na tunabaki kuendesha shughuli kama tuko kwenye mfumo wa mhimili mmoja.
Vyombo hivi kuungana kunatokana na makosa yaliyopo katika uandishi wa katiba kwa kutoangalia jinsi gani mihili hii itaundwa na je nini majukumu ya kila mhimili na unatekelezaje majukumu yetu.
Lakini lipo tatizo kubwa la jinsi gani unaweza kuwezesha mihimili hii ilingane nguvu kwa maana hakuna mhimili unaoulalia mwingine. Hapa lazima twende mbali zaidi kwa kuangalia vitu kama fedha na nguvu nyingine.
Kuchukua mhimili mmoja ukaupa nguvu za kwenye makaratasi na ukaupa nguvu halisi ambazo ni fedha na jeshi na mihimili mingine ikabaki na nguvu za kwenye makaratasi tu tayarai hapa checks and balansi imeondoka.
Hapa nazungumza serikali kumiliki nguvu za kiuchumi na kijeshi inaipa nguvu ya ziada kuzilalia mihimili zingine. Hata kama Mahakama wakitoa hukumu kama serikali ndio inatakiwa kutekeleza maamuzi ya mahakama na haijatekeleza je mahakama watafanya nini?
Hata kama bunge litafanya maamuzi kama serikali haijatekeleza maamuzi watafanya nini?
Lengo la kuweka checks and balansi ni kuhakikisha Yule anayekosea anaposolewa na mihimili mingine anatiii kutokana na pengine nguvu ya hawa wawili waliobaki kwa pamoja kumzidi.
Hivyo ni vema katiba ikaondoa utegemezi wa muhimili mmmoja kifedha kwa mhihili mwingine, ni vema katiba ikaondoa pia utegemezi wa maamuzi ya ndani kutoka mhimili mwingine isipokuwa mambo ya utungaji wa sera za nchi, sheria lakini si kwa mambo ya kiutendaji kama kupata watumishi na mengine.
Lakini ipo nguvu kubwa sana ya jamii ambayo ni jeshi la kulinda mipaka ya nchi.
Katika dhana ya kutengeneza checks and balansi na kuangalia usalama wan chi ni vema jeshi la wananchi likawekwa moja kwa moja kwa wananchi wenyewe kwa maana ya kuliweka chini ya bunge.
Kuliweka jeshi mikononi mwa serikali inaweka utawala wa nchi katika mfumo wa kifalme ambao wananchi hawana mamlaka bali kila kitu anaamua mfalme wao na huyu hachaguliwi na wananchi bali waliamini amechaguliwa na miungu hivyo wananchi hawana maamuzi bali miungu itawaamulia kupitia kiongozi au mfalme wao.
Kuliweka jeshi mikononi mwa serikali inaipa serikali nguvu za kifalme kwa kujiamlia mambo inavyotaka yenyewe na hakuna wa kusema tofauti na wanavyotaka na watataumia nguvu za majeshi waliyonayo kulazimisha maamuzi yao.
Lakini ukiliweka jeshi mikononi mwa bunge lakini jeshi hili likabaki kutojihusisha na shughuli za kawaida bali linaweza kutumika katika hali ya dharura, hapa unakuwa umerejesha nguvu hii kubwa mikononi mwa wananchi kwa maana kwenye chombo chao cha kufanya maamuzi badala yao.
Katika mfumo kama huu ni rahisi kupata cheksi and balansi katika mihimili kwa mihimili kubaki kusuaguana kwa hoja na anayeshindwa anabaki kusikiliza wenzake wamemwambia nini.
Kukisha patikana checks and balansi katika mihimili juu ilivyo kaa basi kinachofuata ni kuweka utaratibu mzuri wa majukumu katika kila mhimili ili kuiwezesha mihimili yenyewe kutimiza majukumu yake kwa kutumia ujuzi na maarifa, kuondoa uwezekano wa wajinga kutumia nguvu hizi za mihimili kufanya maamuzi kulingana na upumbavu wao. Mfano katika hali kama hiyo ni lazima bunge lijengwe kutumia ujuzi na utaalamu katika kusimamia serikali. Hapa kunaweza kuanishwa aina ya wabunge, majukumu ya wabunge, utaratibu wao wa kufanya kazi na mimi ningesema ni bora vyama vya wabunge vibaki milangoni wakiingia bungeni na bunge linakuwa moja kuhoji serikali. Mabishano ya vyama vya siasa yanaweza kuhamishiwa TCD lakini bungeni serikali kwa waziri kuwana wataalamu wake wakijibu hoja kwa upande mmoja na wabunge kwa upande wa pili.
Matatizo yote unayoyazungumza kuhusu gongo, unga na mengine nashindwa kuelewa yanatokana na mihimili hiyo kutokufanya kazi yake ipasavyo na yale niliyoyaainisha hapo juu ndiyo sababu kuu lakini na wewe unaweza kuchangia ili tujadili. Kwa nini nasema hivyo? Serikali ndiyo yenye jukumu la kudhibiti mambo hayo, sasa inafanya nini? Kodi zetu zinatakiwa kutumika kutoa elimu, kutengeneza taasisi, kuajiri wataalamu wa kupambana na haya. Yapo mambo mengi yanategemea katika maswala haya hivyo tunatakiwa kuisikiliza serikali inafanya nini na tupime kama inatimiza wajibu wake au la.
Sasa wewe unatakiwa kutambua kuwa ni mambo gani mwananchi amekasimu madaraka yake kwa bunge? Ni madaraka haya yote yamekasimiwa kwa bunge. Bunge ndilo linatakiwa kufanya kazi hii badala yetu sisi wananchi kuangalia kama serikali wanatimiza wajibu wao. Sasa je bunge wanafanya kazi hiyo? Kazi ya mbunge si kujenga shule na barabara bali ni kusimamia serikali.
Kwa mwananchi madaraka yaliyobaki kwangu ni kufanya maamuzi ya mwisho ambayo ni kupiga kura kwa maana kama mwisho sidharidhika na utendaji wa serikali nawajibisha, kama sijaridhika na utendaji wa mwakilishi wangu ninawajisha, kama nikilidhika na mipango ya maendeleo nachagua , kama nikiridhika na mipango, mbinu na hari ya mwakilishi wangu namchagua.
Kakini elimu yetu ya uraia haitujengi katika sisi sote kutambua majukumu na wajibu wa kila mmoja wetu bali kila mtu ana uelewa wa kwake na kila mtu anafanya anavyotaka yeye.
Matokeo yake ni sote kujikuta tuko uwanjani tukicheza mpira lakini sote hakuna anayejua gori lake ni lipi na la adui yake ni lipi bali tunabutua mbira tu. Ukifika mbele yako unabutua tukisikia gori ndio tunasikiliza na hapo ndio tunabaini na nani kafunga na nani kafungwa.
Katiba ndio msingi wa maisha ya watu wake na tunaweza kuanzia hapo kuweka mifumo yetu sawa.
Bila kuweka mifumo sawa tukategemea kubutua tu tunakuwa tumerudi katika mifumo ya maisha ya zamani ya watu ambao walikuwa hawana utaalamu wowote bali kila kitu wanabahatisha. Mtoto akiumwa hujui sababu wala tiba unachuma kila mti unajaribu kumpa na kufanya kila aina ya kinachowezekana. Kw wale waliobahatisha kuchuma mti sahihi wagonjwa wao walipona na wakaukumbuka mti huo na hiyo iliwapunguzia ukali wa maisha kwani kwa kila aliyeumwa hawakuhainga kujaribu miti yote tena bali kama mazingira yanafanana wanampa mti ule ule. Hii imetusaidia mpaka leo hii kwani madawa mengi yalivumbuliwa kwa mtindo huo lakini wao walihangaika sana.
Kwetu sisi tunayo matatizo ambayo tunataka kukabiliana nayo, tutakuwa wapumbavu kama tutaendelea kugangania katika njia ya kubahatisha bahatisha, kubutua tu huku tukiwa hatujui sababu tunafunga wapi.
Wenzetu walikwisha pita huku hivyo tujifunze kwao ila tusiangalie jambo moja kwa maana ukiangalia mfumo wa utengenezaji wa mihimili kwa wenzako na bila kuangalia mifumo yote unaweza kupotea. Tuchukue basics ambazo ni kama checks anda balansi na kuangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kuzitengeneza katika mazingira yetu.
Marekani au Kenya raisi anaweza kuteua kiongozi wa Mahakama pengine kutokana na mifumo yao wakapata checks and balansi lakini kwetu sisi tukiweka mfumo huo kama hatuna mfumo wa kudhibiti mtu asiteue rafiki yake, ndugu yake, mshirika wake hatuwezi kupata cheksi and balansi.
Kwa maana nyingine kutobutua ni kuangalia mifumo ya wenzetu na kuiboresha ili ifanye kazi katika mazingira yetu au tuifanye itutatulie matatizo yetu.
acha kumezeshwa maneno na wachumiatumbo waliokutuma humu jenga hoja unataka mifumo gani hiyo? Usichokielewa ni nini hujasoma katiba pendekezwa imeweka wazi mifumo mizuri ya utawala nchini kunazia serikali,mahakama na bunge,najua unatamani sana kuona tz inakua na utawala wa kambare eti na wewe uwe unafanya uteuzi haiwezekani lazima ukubali,sio kila unaloliwaza litaingia kwenye katiba itakua sio katiba hiyo ni tungo za abunuwazi, mfumo wa kusimamiana ni watu kujitambua na kufanya maamuzi sahihi na sio kulalama kama wewe unayekaa na wauza gongo,wauza vitu feki afu unategemea katiba iwakamate bila wewe kujua wajibu wako