G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 165
- 100
✍#GMdadisi
Sijui ni lini WAFUGAJI na WAKULIMA watakuja kuelewana na waishi pamoja bila kuwa na migogoro wala chuki. Nadhani hii yaweza kuwa ni ndoto nzuri ambayo haitakuja kushudiwa katika kizazi hiki.
Bahati mbaya sana ukimsikiliza mfugaji analalamika kuonewa na mkulima. Vivo hivyo mkulima analalamika kuonewa na mfugaji. Kiufupi kila mmoja anajiona mwenye haki mbele ya mwenzake.
Yaaan popote alipo mkulima, mfugaji hawezi kuishi kwa amani. Na alipo mfugaji mkulima ataishi kwa wasiwasi tu siku zote labda akishavuna.🤭
Kuna haja hawa watu wawekewe mazingira ya kutoingiliana kwani kila mmoja anatafta kukidhi malengo yake ambayo kukaa karibu karibu haiwezekani.
Mkulima anathamini zaidi mazao yake na kuona mifugo si lolote kwenye maisha, huku mfugaji akiamini katika mifugo yake na kumuona mkulima ni mpotezaji tu wakati wote na hata thamani yoyote mbele ya mifugo yake.
Mkulima wa kule Kasato, Ruganzu, Ntungamo, Runazi na hata Katunguru mawazo yake ni sawa sawa na mkulimà wa Kinowe,Micheweni, na mfugaji wa Micheweni ana mawazo sawa na mfugaji wa Rukoke, Nyakahura..nk.
Hivyo ili kuepusha migogoro kama hii, ni muhimu wafugaji wachangamane na wafugaji wenzao, huku wakulima pia wakae na wakulima wenzao.
Vinginevyo hata wale wamasai waliopelekwa kule MSOMERA, Tanga kama wataingiliana na wakulima tutakuwa tumeongeza idadi ya migogoro ambayo hata kama si leo basi kesho au keshokutwa utaibuka tu.