Sasa kama mnajua kuwa GSM ambao ndiyo Wadhamini Wakuu wa Yanga SC na kwamba itasababisha Fikra zenu za Kipumbavu kuwa kutakuwa na Upangaji wa Matokeo (Match Fixing) pale Yanga SC ikicheza na hivyo Vilabu Saba ( 7 ) sasa kwanini nanyi / nasi pia tusimwambie Tajiri yetu Tapeli na Muongo nae amalizie kwa Kuvidhamini hivyo Vilabu vingine Saba au Nane vilvyobaki ili nasi tupange Matokeo tuwe Mabingwa?
Hamna Akili kabisa nyie yaani mnaacha / tunaacha Kulia na Uozo mkubwa unaoanzia katika Uongozi, Benchi la Ufundi, Wachezaji na hata Sisi Mashabiki / Wanachama tunaanza Kukimbilia kusema kuwa GSM na Yanga SC wanapanga Matokeo kwa Kuvinunua Vilabu na mpaka Waamuzi wa Ligi Kuu.
Hebu Mashabiki Wenzangu wa Simba SC nawaombeni Leo tuweke Unafiki na Upumbavu wetu pembeni na tuulizane haya Maswali. Hivi kweli tukitulia kabisa tukiwaangalia Wachezaji wa Yanga SC, Makocha wao, Utawala / Uongozi Wao, Mfumo wao mzima wa Kiutendaji, Idara zao zilivyo,Ufanisi na Morali yao kuanzia kwa Mashabiki hadi Mashabiki walionao unafanana na Sisi Simba SC yetu?
Soma Pia: Mdhamini mkuu wa Yanga GSM kudhamini timu nyingine saba za ligi kuu siyo fair
Kiutani wetu wa Simba na Yanga Mimi GENTAMYCINE huwa napenda sana Kuwatania wana Yanga SC wote hapa JamiiForums ili tu Kuchangamshana na Kudumisha ule Utamaduni wetu wa Utani wa Jadi ila kiukweli na nikivaa sasa Viatu vya Mwanamichezo na Mchambuzi na ambaye pia naijua Sayansi ya Mpira ilivyo siogopi na wala sioni Aibu kusema kuwa Yanga SC wameshatuacha mbali, wapo vyema, wanajua wanachokifanya, wala hawahongi Waamuzi au TFF bali Continuity Performance yao ndiyo inawabeba.
Mwisho nashauri huu muda ambao Sisi Wapuuzi ( wana Simba SC nami GENTAMYCINE nikiwemo ) ambao Kutwa tunautumia Kuwalaumu GSM na Klabu ya Yanga kuwa Wanahonga tuutumie Kuuhoji Uongozi wetu kuwa ni kwanini kila mwaka wanafanya betting katika Usajili wa Wachezaji wetu na pia kwanini Klabu ya Simba inaendeshwa Kienyeji Kienyeji, Kishikaji, Kiunafiki na kuna Wapigaji ( Wazee wa 10% wengi sana ) na hakuna Umoja baina ya Uongozi na Sisi Mashabiki?
GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mzee wa DOZI TUKUKA nimemaliza na kwa wale ambao MTANICHUKIA kwa huu Ukweli wangu wala sijali, ila Siku zote nitabakia kuwa Mkweli, Muwazi na kamwe sitokubali kuwa Mnafiki au Muongo ili tu niitetee Klabu yangu ambayo kila Siku naiona inadidimia tu huku Wapuuzi wengi wakiwa wala hawalioni hilo na badala yake Wanadanganywa tu na Comedy za Msemaji wetu wa hovyo.
Tujitafakari na Tujitathmini sana kwani bado hatujachelewa japo kwa kuwa Mabingwa Msimu huu tumeshachelewa.