Raelish
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 489
- 162
Habarin wapendwa!! Maisha ni fumbo zito sana, narudi hatua kadhaa nyuma najaribu kuangalia jinsi nilivyopoteza tumain kt maisha yangu, kila mlango ulikuwa umejifunga tena na kufuli nzito ya chuma na matumain ya kupata funguo hazikuwepo kabisa. Ni hivi nilibahitika kupata chuo cha diploma ya udaktari(clinical officer) lakin nilikuwa sina kabisa uhakika wa kwenda chuon, hali ya familia ni duni. Mara nyingi nimefika hapa jukwaan kujaribu kuomba msaada huku nikijitahd kujieleza lakn bado sikupata tumain zaid ya kukashifu mtiririko wangu wa uandishi pamoja na kujieleza kuwa natumia mchina, nikawapm watu mbalimbal maarufu humu jamvin lakn sikupata tumain,nikatafuta e.mail za wabunge mbalimbal bado sikupata tumain, nikaingia kt maofisi ya wakurugenz bado sikupata tumain.. ndipo akajitokeza mama mmoja akasema 'nitakusaidia' na ht sikutegemea.. na kweli amenisaidia na sasa nipo chuon ST.BAKHITA. huyu mama ananilipia ada tu amenambia matumiz na mengine machache nijitahd mwenyewe.. ni mtihan kwangu... itaendelea