Kamwe usimuoneshe mteja huitaji pesa yake

masai dada

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
16,207
Reaction score
14,343
Usimuoneshe mteja wewe ni tajiri, usimuoneshe umejipata. Siku zote muoneshe unahitaji hiyo ela yake kuliko oxygen. Usimuoneshe Mteja umejipata

Hata kama kwa siku unafunga hesabu ya milion kadhaa Mteja wa elfu 50 ndo anaikamilisha milioni moja
Milioni moja bila elfu 50 ni 950,000/= Sisemi umnyenyekee mteja au lahh

Ila biashara nyingi/huduma nyingi mnazofanya mnawaonesha wateja mmejipata Nyie wamiliki pamoja na mnaowaajiri

NB;Mpaka leo Bakhresa anauza maandazi na kila shilingi ina thamani.
 
Kipindi nafanya biashara ya magodoro kuna jamaa alishawahi kuja kuulizia godoro, nikamtajia bei [180k] akasema napiga mno nishushe kidogo...

Nkamwuliza una sh ngapi akasema ana [140k] nkamsoma nikagundua hana pesa, Then nkamwambia lipia uchukue, Aisee alijikanyaga pale hadi nkamuonea huruma, nkamwambia aende...

Sometimes wateja wenyewe hua wanatutaka tuwajibu vibaya, Hekima inahitajika saana...
 
Mtu anakuja kuulizi duka zima ila hanununi
Mi nawatreat wateja woote sawa
Wengi wanajikuta wananua tu
Kiukweli siachi ela
 
Ndugu yangu
Bongo huduma ni mbovu
Mpaka basi
Ukisogea tu hapo kwa ruto utajionea tofauti kubwa sana kwenye kutoa huduma
Mtu anafanya biashara lakini ukienda pale anakuonesha hana shida kabisa na hiyo ela yako
Kwa huduma atakayokupa
Sijui ni uzoefu wangu tu au vipi lakini nafikiri wanawake wana hii changamoto zaidi. Kuna dada mmoja wakala maeneo ya mtaani kwetu nishaacha kabisa kwenda kufanya mihamala kwake.

Ana laptop yake pale ofisini kwake, anakuhudumia mteja huku yupo bize na movie, yaani anashindwa hata kuweka movie pause kwanza amalizane na mteja.

Siku aliyoniletea huo ujinga mimi nilimchana live na sijawahi kurudi tena pale ofisini kwake mpaka leo
 
Kuna kipindi nilikuwa nakaa kwenye ki hardware changu akaja mteja kununua vifaa akawa anitajia vifaa nikawa naandika mahali ili nimpigie hesabu alinitajia vifaa karibia duka zima na akaondoka huku nikiendelea kumpigia hesabu.. biashara ni uvumilivu na hekima na kujishusha
 
Kuna wapuuzi nilienda kutuma 5000 walinikalisha muda mrefu kisa kuhudumia wanaotuma kiasi kikubwa hata kwa wale walionikuta
 
Ndugu yangu
Bongo huduma ni mbovu
Mpaka basi
Ukisogea tu hapo kwa ruto utajionea tofauti kubwa sana kwenye kutoa huduma
Mtu anafanya biashara lakini ukienda pale anakuonesha hana shida kabisa na hiyo ela yako
Kwa huduma atakayokupa
Umezungumza point sana, kuna siku nilikua na mawasiliano na mtu wa Taiwani alikua ana promot bidhaa zao kwenye masoko ya afrika haswa huku mashariki, binafsi nilimpa maelezo mengi juu ya masoko ya Tanzania kwa bidhaa zao, alifanikiwa kupata wateja.

Siku alitaka kutembela Tanzania na alikua ananipa info, ila alikosa ushirikiano kabisa na wafanyabishara wa tanzania badala yake alikwenda kenya na alifanikiwa mno , sasa hivi wao na kenya wanafanya biashara sana, ila sisi kwenye lugha ya biashara tupo duni sana.
 
Kipindi nafanya biashara ya magodoro kuna jamaa alishawahi kuja kuulizia godoro, nikamtajia bei [180k] akasema napiga mno nishushe kidogo...

Nkamwuliza una sh ngapi akasema ana [140k] nkamsoma nikagundua hana pesa, Then nkamwambia lipia uchukue, Aisee alijikanyaga pale hadi nkamuonea huruma, nkamwambia aende...

Sometimes wateja wenyewe hua wanatutaka tuwajibu vibaya, Hekima inahitajika saana...
Hii inatokea sana mtu kataja bei yake unamwambia alipie bado hana alafu kashakutupia lawama.
 
Sijui ni uzoefu wangu tu au vipi lakini nafikiri wanawake wana hii changamoto zaidi. Kuna dada mmoja wakala maeneo ya mtaani kwetu nishaacha kabisa kwenda kufanya mihamala kwake.

Ana laptop yake pale ofisini kwake, anakuhudumia mteja huku yupo bize na movie, yaani anashindwa hata kuweka movie pause kwanza amalizane na mteja.

Siku aliyoniletea huo ujinga mimi nilimchana live na sijawahi kurudi tena pale ofisini kwake mpaka leo
Unakuta ameajiriwa
Na boss wake yupo ofsi nyingine au kawekwa na mume wake

Wengi hawana uchungu na kupoteza mteja au pesa
 
Back
Top Bottom