Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sijakataa kwamba ni utamaduni.Kiranga jamani.
Mahari ni utamaduni unaomba ridhaa kwa wakwe zako kuwa unaoa na utamtunza mke na watoto wote watakaopatikana kwenye nyumba yenu.
Kamwe mahari haiwezi kumfanya mwanamke awe bidhaa
Kuwa utamaduni hakuondoi ukweli kwamba ni utamaduni unaomfanya mwanamke kuwa bidhaa.
Na kuna watu wakiona bidhaa haifai, wakimpa mwanamke talaka, wanadai sehemu ya mahari waliyolipa.
Huko Africa hususan, kitu kuwa utamaduni haimaanishi ni kizuri.
Kuna sehemu nyingi bado wanawake wanakatwa visimi kwa minajili ya utamaduni. Huu ni utamaduni, lakini si mzuri.
Ukisoma tamaduni za Africa, kihistoria, mwanamke na mtoto ni kama mali za mwanamme tu.
Na ndiyo maana machifu walikuwa na wake wengi, watoto wengi. Ni alama ya utajiri.
Na kwa kuwa mwanamke ni bidhaa kwa tamaduni hizi, basi anawekewa bei rasmi.
Na bei hiyo inaitwa mahari.
Jamii yenye mahari haiwezi kuwa na usawa wa watu.
Anayelipa mahari, ceteris paribus, atajiona yuko juu kwenye ndoa.
Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni mtumwa wa mwanamme, sina tatizo nawe.
Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni sawa na mwanamme kiutu, hapo naona kuna uongo.
Kwa sababu kama mahari ni utamaduni wa zawadi tu, kwa nini familia ya mwanamme haipewi zawadi ikawa mwanamme anatoa mahari kwa mwanamke na mwanamke anatoa mahari kwa mwanamme? Mahari iwe exchange of gifts tu?
After all, reciprocity is the height of diplomacy and love.
Mahari ni bei ya kununua mke.
Inawezekana ni kitu muhimu katika jamii masikini, kuzuia watu masikini wasioweza ku maintain family kuoa.
Lakini, kwenye jamii zilizovuka mto huo, boti hilo halihitajiki.
Ndiyo maana jamii zilizoendelea kielimu na kiuchumi zimeondokana na utamaduni huu.
Lakini labda huko Africa tunauhitaji bado.
Hayo yote hayabadilishi ukweli kwamba mahari ni bei ya kununua mke kama bidhaa.