Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Winnie Kilemo kuna vitu huwa anaandika huko facebook hadi namwonea huruma,,,, wakati flani namwona kama mtu aliyekaa kwenye wokovu miaka mingi ila ni mchanga kwenye mambo ya kiroho (kifalme)!.......


mi nadhani angeaza kwa kushauri wazazi kutopanga mahari kubwa sana , au angeshauri mabinti wanaoposwa wawambie wazazi wao kwamba mtarajiwa wangu hana uwezo kwaio msipange mahari kubwa!


anyway, ukitumia biblia, anaetakiwa kulipiwa mahari ni binti kigori tu....... ndivyo torati inavyoeleza!..... ukikuta sio kigori warudishie wenye mtoto nao warudishe mahari!
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.


Na
Winnie Kilemo
Ukisoma visa vya kulipa mahari kwenye biblia, kama umesoma kweli ,ilikuwa kama adhabu
 
Winnie Kilemo kuna vitu huwa anaandika huko facebook hadi namwonea huruma,,,, wakati flani namwona kama mtu aliyekaa kwenye wokovu miaka mingi ila ni mchanga kwenye mambo ya kiroho (kifalme)!.......


mi nadhani angeaza kwa kushauri wazazi kutopanga mahari kubwa sana , au angeshauri mabinti wanaoposwa wawambie wazazi wao kwamba mtarajiwa wangu hana uwezo kwaio msipange mahari kubwa!


anyway, ukitumia biblia, anaetakiwa kulipiwa mahari ni binti kigori tu....... ndivyo torati inavyoeleza!..... ukikuta sio kigori warudishie wenye mtoto nao warudishe mahari!
Mbona mahari zinazopangwa ni za kawaida kabisa.

Wanaume wenyewe ndiyo wasatoaji wazuri wa hizo bikra za wanawake.
Zamani wanaume walikuwa watulivu.
 
Na wengi wanaojilipia mahari ndoa zimewatokea puani, wameishiwa kuuliwa tu, na kuteswa Hadi kuachwa walemavu, mwanaume asiyeweza kutoa mahari na asioe kabisa aisee mpaka awe vizuri
 
Ni kweli kabisa. Mahari ni ujumbe wa kuomba ridhaa ya kuishi na mtoto wa kike.

Mahari ni jambo lisilo na utata katika kulijadili. Unapopenda mtoto wa mtu usiogope kwenda kuomba ridhaa. Najua maisha ni magumu, unajiona hauna hadhi ya kwenda kwa wazazi wa mtu kuomba ridhaa ya kuishi na binti yao.

Mahari kwa asili yake si gharama ya kutoa kwenye mfuko wa mwanaume bali ni swala la familia ya mwanaume.... Wajomba na baba wadogo kwa wakubwa, makaka, baba na mama watajikusanya kisha watamsapoti kijana wao kwenda kuposa. Tatizo familia za siku hizi hazina ushirikiano na wazazi wanawaachia watoto wadeal na mambo yao on their own ndio maana majanga ni mengi.

Ukikosa msaada wa familia yako hata rafiki na jamaa wanatosha kukupa sapoti. Washirikishe waje kukusaidia kuipata mahari. Na mahari haitolewi yote ukiambiwa milioni hata laki tano unapeleka, sasa why ufeli?!

Toa mahari, kisha tuma wazee wawanong'oneze ukweni kuwa harusi itasubiri kidogo mnaendelea kujipanga.


Maisha ukiyachukulia kwa standard ya juu huwa ni magumu sana kuyaanza, ila ukiyachukulia kwa uhalisia yanawezekana sana na nimepesi. Usiogope kupambana kupata unachotaka. Washirikishe ndugu na jamaa wa karibu wakusaidie.
Kumbe mahari inachangwa na wazazi?
 
Huyo uliyemnukuu alilipiwa mahari kiasi gani?

Kuna wazee wakuda wanataja mahari ndefu utadhani wanataka kupata mtaji wa biashara...

Sijui kreti mia za bia, ng'ombe kumi, mbuzi sijui wangapi...
Sijajua alilipiwa kiasi gani
Ila Kuna sehemu amesema alilipiwa
 
Mahari is overrated, mahari kwa dunia ya sasa haina maana yoyote. Kwani zamani walitoa mahari kwa sababu zipi, I thought ni asante kwa wazazi kimtunza binti yao hadi anaolewa akiwa kigori(kigoli).

Leo unaoa mke wa watu huko, walishajitwalia wengi kabla yako wewe unakuja kuhalalishwa tu na kujibebea, kuongeza laana katika uzao wako.

Mahari for the purity nakubali, Ila kwa sisi tuliojiharibu, sioni mantiki hata kidogo.
Ina maana na huwezi kuoa bila mahari mkuu.
Hata Sasa mahari ni Akhsante kwa wazazi
 
Kulipia mahari kwa lugha kamili ya Kiswahili ni kununua mtu.
Sasa ole wako nikununue alafu ukumbuke kwenu! Nina mamlaka ya kuifanya bidhaa yangu niliyoinunua kwa pesa yangu vile nitakavyo
 
Mahari haitakiwi kuwa kiasi ambacho bwana harusi anashindwa kulipa in the first place.
Ndio maana kwa wenzetu waislam, bibi harusi ndie anaeseti kiwango cha mahari (Hivyo, kwa sababu anafahamu uwezo wa mwenzi wake hawezi kuseti kiwango ambacho kitamtesa mwenzi wake).
Mfano, bi harusi anaweza kusema yeye mahari anayoitaka ni kitabu cha quran tuu, au kikombe.
That is how is supposed to be. Achana na trend za siku hizi ambapo mahari inawekwa kama gharama ya kumnunua binti kiasi cha kuumiza kichwa vijana waoaji.
Hata Kwetu wakristo mahari huwa ni ya kawaida sana.
Na baadhi ya makabila vitu hutolewa Sana kuliko pesa..yaani pesa itakuwa kidogo tu.
 
Una-discuss issue ya mahari,je huyo anayepaswa kutolewa hayo mahari anazo sifa za kukaa chini na washenga yakajadiliwa hayo.

Maana mabinti wengine wameshatumika kiasi mahari itabidi watoe baba zao na kuwapa asante wale vijana watakaosaidia kuchukua binti zao.
Yaani baba zao watoe mahari??
Mke wa hivyo huwezi kupata mkuu
 
kwa namna mlivyotumika bado tu mnahitaji mahari? kwa mantiki hii mnataka muendelee kuwa singo maza wa kudumu
Kama wewe huwezi kuoa acha wenzio wataoa.
Hakuna mke utakayegawiwa bure.
 
Hili neno 'mahari' mmelikuza sana nyakati hizi, utakuta unatajiwa mahari kubwa kama vile unalipishwa fidia.

Nadhani hali ya kiuchumi huchangia hili.
 
Back
Top Bottom