Kamwe usisikilize mziki na kuufia kama huna uhakika na usafi wa wasanii wa muziki huo!

Kamwe usisikilize mziki na kuufia kama huna uhakika na usafi wa wasanii wa muziki huo!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,902
Wengi mtaona ni ujinga mkubwa huu lakini najua nachoandika hapa. Epuka sana kufia mziki wowote ambao wasanii wake sio watu sawa katika maisha yao kiroho. Haswa mbaya ni kama muziki huo umetungwa na wale waliofanya ushirika na ulimwengu wa giza kupata umaarufu kisanii. Vijana wengi ni misukule inayotembea mtaani na watu hawana habari kwanini mambo yapo hivyo.

Hili jambo linafanyaje kazi? Tutajadili kama nikipata nafasi.

Kuna siku nilisikiliza kibao flani nikiwa nchi flani, mara moja niliingiwa na kitu kibaya mno kilichonitesa masaa 24 hivi ila kwa kuwa tu nilijua nini cha kufanya nikafanikiwa kujinasua la sivyo nilikuwa kama mtu anayetumbukia kwenye shimo lisilo na mwisho. Nilijua siku hiyo kuwa sio kila muziki ni salama. Kuwa makini sana na vitu hivyo vipo vingi sana siku hizi!
 
chukua ujumbe ukiupenda basi,, maswala ya background ya mtu hata hawa wachungaji na mashehe tukisema tuwafatilie tutaacha kwenda nyumba za ibada.
 
Hata kiongozi anayeteka watu hafai kuendelea kuongoza.Hivyohivyo na msanii anayeimba nyinbo nzuri lakini matendo yake ni ya hovyo hafai kabisa kuendelea kuimba
 
Back
Top Bottom