TANZIA Kanali Fabian Massawe, aliyekuwa RC Kagera afariki dunia

TANZIA Kanali Fabian Massawe, aliyekuwa RC Kagera afariki dunia

RIP. Amekufa akiwa na cheo kipi Jeshini, Kanali au Luteni Jenerali?
Hapa hata mimi sijaelewa au jamaa alisahau ku edit inakuwaje mtu amestaafu alafu aendelee kupanda vyeo anakua kama museven amejipachika ma vyeo tu au kanal gadafi mbona mwenzao kagame alikua meja na hatumii hicho cheo kwenye siasa zake
 
nakumbuka nilipoanza form1 1995 mzee wangu alilipa ada mwaka uliofuata 1996 sikulipa ada mpaka namaliza shule kwasababu tu Mr masawe aligundua nina kipaji cha kucheza basketball huyy mzee aliibua vipaj vingi na amesaidia wengi kutimiza ndoto zao,Jitegemee ilishehen kila aina ya wanamichezo kuanzia mpira wa miguu,maigizo,ngoma mpaka masumbwi...hawa ni baadhi ya watu maarufu waliolelewa na masawe..Njohole,ally mayai,eddo Kumwembe,solo thang,soggy doggy,Bad gear(.witness,richone,daz mwalimu,DazP,Mh Temba,kajala masanja(basketballer),kisoky,Iddy ligongo,emmanuel Ambrose,chid benz,Gervas kasiga(Director wa movie zote za kanumba na mtunzi wa filamu),wasiwasi mwabulambo(azam tv) etc
Kisocky alikuwa mbele yangu, pia nakumbuka, Kajala pia japo nahisi hakumaliza shule, Ali mayai mchuchu wake alikuwa mbele yangu, Daz baba alikuwa mbele yangu madarasa mawili
 
Mleta uzi mbona baadhi ya mambo uliyoandika yanachanganya ,umesema Kanali , mara unasema alikua Luteni Jenerali, which is which Mtu akishafikia level ya luteni Jenerali sio cheo kidogo , sasa tena bado mnamwita Kanali, alipandishwa vyeo baada ya kutoka kwenye siasa ama alirudishwa jeshini na hakustaafu ama
 
Sasa hawezi kua amefariki akiwa bado kanali,
Huenda kipindi head alikuwa Luteni Kanali, ila sasa hivi kafa akiwa Kanali. Japo toka kitambo hicho alipendeza astaafu hata na Brigedia Geneal. Huenda wenzake walikuwa wanaweka ka uzibe au nae alikuwa na mambo yake, huwezi jua.
 
Si kweli hakuna mtu alikua hana shida na mtu kama Kijazi ila mlishangilia sana kifo chake,

Huyu najua kwanini hamumtukani.
kijazi alikuwa mtu wa karibu na jiwe, Masawe alishastaafu Jeshi na ametumika vyeo vya kisiasa wakati wa JK tu...ni wazi wakati wa JK hakukuwa na chuki kubwa ya kisiasa kama wakati huu wa mungu wa chatoo!.
 
Back
Top Bottom