Kanali Kinana, mtaalamu wa kufukia mashimo. Wapotoshaji watasulubiwa kimya kimya

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Katika karata muhimu CCM waliyocheza ni uteuzi wa Kanali Kinana katika nafasi ya Umakamu mwenyekiti, uwepo wa Kinana ni kuhahakisha ushindi kwa chaguzi zijazo.

Ukiachana na sifa nyingine nyingi na za kutukuka katika utendaji na uongozi hasa ile ya uchapakazi lakini Kanali Kinana anaonekana ni mtaalamu wa kufukia mashimo.

Mashimo ninayoyaona ambayo mzee Kinana ataanza kuyafukia ni kama ifuatavyo:
i) Upotoshaji wa taarifa mitandaoni
ii) Chama kukosa coordination
iii) Chama kukosa ushawishi
iv) Hofu ya kushindwa kuzungumza
v)n.k.

Kwa hayo machache hakika kilio cha wapotosha taarifa kitasikika, wanaojiona miungu watu watasulubiwa na watumia nguvu wataumia. Kutakuwa na mabadiliko makubwa serikalini na chamani hususani katika namna watu watakavyokuwa wanatoa kero za wananchi

Aliweza kuyafukia mashimo alipokuwa katibu mkuu wa CCM kuanzia 2012 mpaka 2017 na kusema ukweli alifanikiwa sana, naamini atafanikiwa sasa
 
Huyu Mzee ni mtaalamu wa siasa, sasa tutarajie kuona siasa za kiushindani na ustaarabu, lakini kubwa hili ni chaguo sahihi kwa wakati sahihi kwa CCM kwa wakati huu.
 
Hivi mafanikio gani unayategemea kutoka CCM? Ama nimesoma vibaya!
 
Hapana, hukusoma vibaya, ila mleta mada hakujieleza vizuri.

Kiujumla, mada yake ni fikirishi sana, lakini hakuijengea hoja zinazostahili kujengwa juu ya umuhimu wa Kinana kwenye chama hicho wakati huu.

Kusema kwamba CCM itamtegemea sana huyu mtu wakati huu hadi 2025, itakuwa ni 'understatement' (sijui niandikeje kwa lugha yetu taathimu).

Simwoni mtu mwingine yeyote humo CCM mwenye uwezo wa kuisogeza karibu zaidi CCM kwa wananchi kwa sasa, zaidi ya huyu Kinana.

Ni wazi kabisa, kuwa "ni mfukia Mashimo Mzuri Sana."
 
Baada ya Magufuli kuweka wazi kila kitu, toka uozo ndani ya CCM mpaka serikalini hakuna mwanasiasa yeyote anayeweza kuiponya CCM. CCM inaweza kuponywa na vyombo viwili tu - Jeshi la Polisi na la wananchi TZ (JWTZ). Zaidi ya hapo hakuna, hata mchawi hawezi kufanya lolote.
 
Majeshi yataongezewa budget ili yasijiingize kwenye shughuli za uzalishaji wabakie kufanya mambo ya taaluma zao. Ukweli ni kuwa budget za majeshi ni siri. Lakini kwa akili ya kawaida Polisi kwa mfano wanaweza kuongezewa budget inayo fikia fedha za uchafu wa Tanesco? Tuanzie kwenye makazi yao tuone. Niwapongeze Tanesco na Wizara leo huku kwetu ukanda wa Kidroni umeme umekatika mara moja tu hadi masaa haya.
 
Hata Mangula na Bashiru ulisema hivyo
Huyu Mzee ni mtaalamu wa siasa, sasa tutarajie kuona siasa za kiushindani na ustaarabu, lakini kubwa hili ni chaguo sahihi kwa wakati sahihi kwa CCM kwa wakati huu.
 
Ikawaje Sasa akashindana mwenyewe? Ni ajabu kwa sifa hizo alafu anagombea na kivuli
 
Mfukia mashimo mwenzake😁😁😁
 
Ikawaje Sasa akashindana mwenyewe? Ni ajabu kwa sifa hizo alafu anagombea na kivuli
CCM ni chama makini sana na zaidi ya yote utaratibu huo wa kupigia kura mmoja kwa CCM ni demokrasia ya hali ya juu sana. Kwa nini?

Mgombea ambaye hana mpinzani akipitishwa kugombea ni sharti apate theluthi mbili au zaidi ya kura zote na kushindwa kupata kiwango hicho anaondokana na sifa za kugombea nafasi hiyo ikitokea kashindwa.
 
Hii ni sawa na kusema kuna watu wanafanya watakalo kwa sababu kuna watakao fukia mashimo.
Kweli siasa ni sanaa siyo sayansi.
 
Baada ya Magufuli kuweka wazi kila kitu, toka uozo ndani ya CCM mpaka serikalini hakuna mwanasiasa yeyote anayeweza kuiponya CCM. CCM inaweza kuponywa na vyombo viwili tu - Jeshi la Polisi na la wananchi TZ (JWTZ). Zaidi ya hapo hakuna, hata mchawi hawezi kufanya lolote.
Mkuu, natamani sana kuamini unayosema, lakini waTanzania nawafahamu vyema kabisa. Kinana, hata Magufuli alimlilia sana asing'atuke, lakini ililazimu iwe hivyo, kwa sababu Kinana asingeweza kufanya kazi kwa utashi wake chini ya Magufuli.

Unajuwa, unapofanya kazi chini ya mfumo usioutaka, hata uwe fundi mzuri vipi huwezi kufanikisha kazi yako utakavyo?

Kinana ni fundi sana. Subiri utaona kama unao uwezo wa kufuatilia vizuri yatakayokuwa yakitokea toka sasa hadi 2025.

Sasa siwezi kutabiri uwezo watakaokuja nao CHADEMA katika kuwafahamisha wananchi juu ya "ufukiaji mashimo" anaoufanya Kinana, huku chini ya ufukiaji huo kukiwa na mahandaki chini yake. Sijui kama CHADEMA wataweza kuifanya kazi hiyo vizuri.

Lakini nisisahau haya maneno ya mwisho uliyotumia katika mistari yako hapo juu, kwamba: "...hakuna mwanasiasa yeyote anayeweza kuiponya CCM, CCM inaweza kuponywa na vyombo viwili tu - POLISI na Jeshi..."

Naona tunatofautiana kidogo kuhusu "KUPONA". Mimi siamini kuwa Kinana anaingia kwenye uongozi kuiponya CCM, ila kuendeleza maslahi ya waliomo ndani ya chama hicho. CCM haiwezi kamwe kupona, kuwa chama tena cha siasa kinachosimamia maslahi ya wananchi.
Hiyo maana yako ya "KUPONA" unayoisema hapa, kultwa na jeshi au polisi, huko siyo kupona. Huko ni kuendelea tu kubakia madarakani kinyume cha matakwa ya wananchi. Atakachoweza kufanya Kinana ni kuwasahaulisha tu kwa muda, wananchi madhira yaliyokwishatokea huko nyuma, ndiyo maana ya "kufukia mashimo" huko.
 
Katika karata muhimu CCM waliyocheza ni uteuzi wa Kanali Kinana katika nafasi ya Umakamu mwenyekiti, uwepo wa Kinana ni kuhahakisha ushindi kwa chaguzi zijazo.

Ukiachana na sifa nyingine nyingi na za kutukuka katika utendaji na uongozi hasa ile ya uchapakazi lakini Kanali Kinana anaonekana ni mtaalamu wa kufukia mashimo.

Mashimo ninayoyaona ambayo mzee Kinana ataanza kuyafukia ni kama ifuatavyo:
i) Upotoshaji wa taarifa mitandaoni
ii) Chama kukosa coordination
iii) Chama kukosa ushawishi
iv) Hofu ya kushindwa kuzungumza
v)n.k.

Kwa hayo machache hakika kilio cha wapotosha taarifa kitasikika, wanaojiona miungu watu watasulubiwa na watumia nguvu wataumia. Kutakuwa na mabadiliko makubwa serikalini na chamani hususani katika namna watu watakavyokuwa wanatoa kero za wananchi

Aliweza kuyafukia mashimo alipokuwa katibu mkuu wa CCM kuanzia 2012 mpaka 2017 na kusema ukweli alifanikiwa sana, naamini atafanikiwa sasa
Hii nchi masikini Sana na watu wake masikini
 
Back
Top Bottom