Kanali Martini Mkisi kweli maisha ni gwaride

wakati huo hakukuwa na makanali wengi walikuwa wanahesabika. Major ndiyo ilikuwa kikomo kwa wengi; mmarufi walikuwa ni pamoja na Major Kyusa pamoja na Major Hashim Mbita wakati huo.
Kwa zamani ambapo hata viwango vya upandaji vyeo ilikuwa hauendani na wakati sio mbaya maana ukistaafu kwenye umeja umeja wenyewe kwa wakati huo hupati aibu ya kuwa ulikwama sababu ya mitihani

Ila Leo mtu akistaafia umeja ni evidence ya ukilaza
 
Kuna mzee hapa anasema Mkisi alikuwa brig. miaka ya ' 70 na alikua kiongozi JKT
ukweli ni UPI?
Kuna Mkisi wa zamani ni marehemu kwa sasa ndio aliwahi kuwa Brigedia na alifika pia kuwa meja jenerali huyo alijuwa anaitwa Meja jenerali Nelson Mkisi

Huyu tunaemuongelea hapa ameishia cheo cha kanali
 
Mimi zamani nilikuwa najua kwamba mwanajeshi hawezi kupanda cheo bila nchi husika haipo kwenye vita. Nilijua vita pekee ndo vinaweza kumpatia cheo mwanajeshi.

kuna vyeo unapewa baada ya vita tu mfano field marshal.
 
Kilele9 ,

..Major General Nelson Mkisi alikuwa mkuu wa JKT miaka ya 80.

..baada ya kustaafu nafasi yake ilijazwa na Major General Makame Rashid.

..Makame Rashid alikuwa Kanali na mkuu wa mkoa wa Mbeya.

..Raisi Mwinyi alimpandisha cheo kuwa Major General na kumteua kuwa mkuu wa JKT.
 
Hashim Mbita alikuja kupandishwa baada ya kustaafu au?

Maana mazishi yake nilifuatilia amezikwa akiwa ni Brig Gen mstaafu
Alipandishwa baadaye, na nadhani alipanda kutoka major hadi Brigadier General; kwa sababu sina kumbukumbu hapo katikati kwa yeye kuwa Kanali. Maafisa wengi wa jeshi waasisi waliokuwa na vyeo vya chini na baadaye kutumika kwenye shughuli nje ya jeshi alipandishwa kwa mtindo huo. Hata Sarakikya naye alipandishwa ingawa yeye alikuwa major General nadhani alipandishwa kuwa General. Luteni Alexander Gwebe Nyirenda naye alipandishwa kuwa Brigadier General. Mbita alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kwenye mambo ya kidiplomasia zaidi kuliko jeshi; mara baada ya kutoka kuwa Press Secretary wa Nyerere ndipo alipanda kuwa Major na kupewa kamati ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika; aliendelea huko kwenye diplomacy za Ukombozi hadi kustaafu kwake
 
Kichuguu,

..Captain Mushi aliyekuvutia ukapenda cheo cha Captain ndiye huyu hapa kwenye video?

Sijui sura yake lakini enzi hizo alikuwa vocal sana; baadaye Nyerere alimhamisha kutoka jeshini na kumfanya General manager wa shirica fulani la mbao, sijui TWICO
 
Sijui sura yake lakini enzi hizo alikuwa vocal sana; baadaye Nyerere alimhamisha kutoka jeshini na kumfanya General manager wa shirica fulani la mbao, sijui TWICO

..basi ndiye huyo unayemuona hapo kwenye video.

..unafahamu aliondoka jeshini mwaka gani, kwasababu alikuwa GM wa viwanda vya mbao kwa muda mrefu.
 

..Mirisho Sam Hagai Sarakikya aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Major General.

..wakati wa Tanganyika Rifle Sarakikya ndio alikuwa the most senior among the native officers akiwa na cheo cha Captain.

..baada ya maasi ya Tanganyika Rifles na Mwalimu alipolivunja jeshi hilo na kuunda Jwtz/Tpdf, Sarakikya alipandishwa ngazi kuwa Brigadier na kuteuliwa kuwa cdf wa kwanza wa Jwtz/Tpdf.

..pia mnadhimu mkuu wa kwanza wa Jwtz alikuwa ni Elisha Jairo Kavana ambaye alikuwa Luteni ktk Tanganyika Rifles lakini akapandishwa cheo na kuwa Major ktk Jwtz/Tpdf.

..kuna kitu ambacho kimenishangaza kwamba website ya Jwtz haimtaji Elisha Jairo Kavana miongoni mwa wanadhimu wakuu. Badala yake wametajwa wakina Brigadier.Nkwera, Tumainieli Kiwelu, Imran Kombe, Martin Mwakalindile, Geofrey Sayore, Iddi Gahu, na wengine.

..Alexander Gwebe Nyirenda aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Lt Col. Raisi Mwinyi kwa kutambua mchango wa Alexander Nyirenda alimpandisha cheo na kuwa Brigadier General akiwa tayari ameshastaafu.

..Mirisho Sarakikya naye alipandishwa cheo na Raisi Mkapa toka Major General kuwa General ili alingane na wakuu wengine wastaafu wa jwtz.
 
..basi ndiye huyo unayemuona hapo kwenye video.

..unafahamu aliondoka jeshini mwaka gani, kwasababu alikuwa GM wa viwanda vya mbao kwa muda mrefu.
Alitoka jeshini zamani sana, ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya sabini kabla ya 1975. Kama angelikuwa amebakia Jeshini, alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwa CDF or CoS, kwani alikuwa anajulikana kuwa ni mwanajeshi msomi sana wakati huo.
 
My personal views katika kipindi cha miaka 2016-2020 ni wanajeshi wachache wameludi shule kuongeza elimu ukiachana na course mbali mbali zilizopo ndani ya taasisi yao tunaitaji professors and Doctors wengi ili wajisifu Kama Mkisi...
Nimekumbuka enzi za JITEGEME ukifanya dhambi Kama una mbio kimbia ila wakikushika umeishaa...afande tupatie mbwa vijana wanambio sana hawa ...afande anawajibu nileteeni vijana kwenye team ya riadha[emoji23]
 
Hiyo sijaijua kumbe Mkisi alikuwa anatuma wanajeshi kukamata wanaochochora
 
Cheo cha mwisho ni major jenerali au jenerali? Ebu nyoosha hapo mkuu!!
 
Afande tulia basi dah 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…