Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ametoa wito kwa viongozi na wanasiasa wa mkoa huo kufanya siasa za kistaarabu badala ya siasa za chuki na zinazogawa wananchi akisema hazitavumiliwa mkoani humo.
Kanali Mtambi ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Mara katika kikao kilichoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Lengo la kikao hicho lilikuwa kuwaelimisha viongozi hao kuhusu umuhimu wa kujiepusha na vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao.
Kanali Mtambi amesema baadhi ya viongozi wamekosa sera za maana za kunadi kwa wananchi, na badala yake wamejikita katika "siasa za majitaka" zinazochochea chuki, fitina, ukabila, na kugawa wananchi.
Amehimiza vyama kufuata kanuni na taratibu zilizopo ambazo zinaelekeza namna ya kushughulikia malalamiko yoyote yanayotokea wakati wa uchaguzi.
Amewataka wananchi kutokubali kudanganywa na siasa za namna hiyo, kwani zinaweza kuwanyima fursa ya kupata viongozi wenye sifa na uwezo.
Pia, Soma: MARA: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
Kwa upande wake, Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Mara, Mohammed Sharif, amewasihi viongozi wa kisiasa kuimarisha mikakati ya kutokomeza vitendo vya rushwa ndani ya vyama vyao. Pia amewataka kutoa elimu kwa wafuasi wao kuhusu kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Sharif amesema taasisi hiyo imejipanga kikamilifu kudhibiti mianya yote ya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Soma:
• Kahama: TAKUKURU waonya Chawa wanaotumika kugawa fedha na zawadi ili wagombea wao wachaguliwe
• TAKUKURU hawana meno kwenye rushwa ya uchaguzi wa ndani CCM?