Kangi Lugola alikuwa sahihi kuagiza vifaa kazi vya kisasa vya kuzimia moto, lakini akatumbuliwa kwa sababu zisizo na msingi

Kangi Lugola alikuwa sahihi kuagiza vifaa kazi vya kisasa vya kuzimia moto, lakini akatumbuliwa kwa sababu zisizo na msingi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Tukichukulia tukio moja tu la moto uliotikisa au unaotikisa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tunapata jibu moja kwa moja kuwa ni vyema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likawa na magari na ndege za kisasa za kuzimia moto.

Tanzania tuna hifadhi nyingi, hivyo lolote linaweza kutokea kwenye hizi hifadhi zetu, helicopter za kuzimia moto na kuokoa watu wakati wa majanga ni jambo lisilokwepeka.

Mafuriko yaliyoichapa Tanzania na Afrika Mashariki mwaka jana kuna watu Kilwa walikufa kizembe. Kama tungekuwa na helicopter za uokoaji wasingekufa baadhi ya watu.

Kuna siku nilimsikia Rais akipondea ile tenda ya Lugola na Andengenya, akisema helicopter hazina kazi kwenye uzimaji moto, ikumbukwe kuwa kesho hili kazi yake si tu kuzima moto. Anayetaka kuamini aende YouTube atafute hotuba ya uuzinduzi wa Nyumba za Magereza Ukonga.

Kama kulikuwa na mistake au harufu ya ufisadi tenda ingeendelea na washukiwa wangefikishwa mahali sahihi na si kusitisha tenda ya vifaa muhimu vya kuzimia moto na uokoaji.
 
Kipanya alisema kitaka kupanda chati kisiasa, tengeneza tatizo kisha litatue, yawezekana hata hili lilikuwa planned ila timing ndiyo imekosewa
 
Kweli, helicopter hazina kazi katika uzimaji wa moto. Mbona tunayo majani mengi tu ya miti ambayo zimamoto wetu wanayatumia kufanya kazi hiyo na wanafanikiwa? Hatuwezi kutumia fedha zetu kununua hizo chopa, na ndio maana Kangi alitumbuliwa.
 
Kangi kiuno kilimponza.
Nje anakata mauno,kwenye simu anamponda.Unaponaje kwamfano.
 
Back
Top Bottom