10 Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao wakawaona Wamisri, wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu wakamlilia BWANA. 11Wakamwambia Mose, "Je, ni kwamba hayakuweko makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani?Umetufanyia nini kututoa Misri? 12 Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!'' 13 Mose akawajibu Waisraeli, "Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu BWANA atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. 14 BWANA atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa
kutulia tu.'' 15 Ndipo BWANA akamwambia Mose, "Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. Kutoka 14: 10-15
Mankaa pole sana, naelewa nafasi uliyopo kwa sasa kwani upo
NEUTRAL ZONE huelewi hatima ya baadae. Kwanza naomba uelewe kwamba huu wakati unaopitia ni sehemu ya maisha, wote huwa tunajikuta tupo
NEUTRAL ZONE katika mazingira tofauti. Nimekukumbusha kisa hiki cha wana wa Israeli walipokuwa wanatoka misri kwenda nchi ya ahadi kuna wakati walijikuta wako NEUTRAL ZONE, hawakuelewa hatima yao ya baadae. Lakini Mungu aliwaambie
WASONGE MBELE japokuwa mbele yao kuna bahari. Naamini hata wewe unaona bahari mbele yako lakini nami nakushauri
KUSONGA MBELE kwani kanani yako iko mbele.
Ukweli ni kwamba huyo mtu hakuwa na mapenzi ya kweli kwako yaani hamkuwa na
BALANCED LOVE nae alitambua hilo kwamba wewe unampenda zaidi kuliko yeye anavyokupenda inategemeana na tofauti zenu ambazo yeye aliona hawezi kuchukuliana nazo. Hii hutokea kwa wengi sio wewe tu. Ikitokea kwamba mapenzi hayako balanced ni kwamba mmoja wenu anakuwa mtumwa kwa mwingine (kuburuzana), hivyo basi isingekuwa tofauti na wana waisraeli walipotamani kuendelea kubaki utumwani.
MANKAA, naomba utambue kwamba wewe ni wa dhamani sana hapa duniani, hakuna mwingine kama wewe
"YOU ARE ONLY ONE ON THIS WORLD" na kuna wengi duniani wanatamani kukutana na wewe. Hivyo basi nakushauri kuwa mtulivu katika kipindi hiki na kuweza kuchukua maamuzi sahihi ambayo hayataleta machungu katika maisha yako yote, naelewa wakati huu unapitia machungu, lakini haya ni ya muda mfupi sana ukilinganishi wakati wako mwingine wa maisha. Ilishawahi kutokea kwa binti mmoja habari kama hii, alikuwa akipatiwa ushauri na mama yangu katika kumfariji; lakini baadae yule binti alikuja kuolewa na mwanaume kutoka nje ya nchi (specifically alikuja kwa ajili yake) alimfahamu vipi, sikutaka kujua zaidi.
Vilevile naomba ufahamu kwamba bado kuna wengi wa dhamani ambao wanakupenda na kukujali wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa na marafiki bila kusahau jamii yote ya JF,
we real love you....!!!!
Nakushauri kutumia
KANUNI YA SIKU 21:
http://www2.fiu.edu/~oea/InsightsFall2004/online_library/articles/daily%20activities%20to%20help%20change%20habits.htm
Watafiti waligundua kwamba mwanadamu anao uwezo wa kubadili tabia yeyote ile ndani ya siku 21, hivyo basi ndani ya siku 21 utamsahau kabisa na maisha yataendelea kama kawaida. Kwa sasa nakushauri ujitahidi kutokukutana nae ndani ya siku hizi 21, naelewa ni ngumu lakini ukiweka dhamira ya kweli yawezekana.
Kumbuka kwamba mahusiano yako na mwenza wako yana uhusiano mkubwa sana na maisha yako ya baadae; hivyo basi huu ndiyo wakati wako wa kujenga au kubomoa. Namshukuru Mungu kwa aliowapa maono ya kuanzisha JF kwani naamini kupitia jukwaa hili tunajifunza mengi.
Nakutakia kila la kheri!!!