Kaniambia akiipata kazi mume wake atapiga deki ndani!

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Nimekaa na mke wa mtu nikampa dili kuna sehemu wanahitajika watu kazi ya kutwa data collection 25,000 kwa siku, project ya miezi 2, alichonijibu akasema yupo tayari tena akiipata hiyo kazi huyo mume wake mbona atapiga deki ndani.

Akasema ana rafiki yake kama wanahitajika watu wengi nikamwabia ampigie sasa anamjulisha rafiki yake halafu anamwambia hii dili nikiipata namtaka huyo boss atakayekuwa anatulipa, nikimpata sasa huyu mwanaume ndio atanijua mimi nani!

Yaani mpaka nawaza nisimconnect na jamaa, anaonekana ana kisasi sana na mumewe ndio vile tu hana namna ni mama wa nyumbani.
 
Kama anafanya visasi sio poa, ila kupiga deki ndani mwanaume unapiga tu, sio hadi mkeo apate kazi.

Au mume kudeki ndani ni jambo baya sana?
 
Ama kweli umaskini mbaya sana, 25k anaona hela nyingi. Hata saidia fundi siku hizi wanapata hizo. Yaani umdharau mtu kwa kulipwa tuhela huto tena twa msimu loh
 
Mwanamke hatariiii ONYO
 
Watu tunalipwa per diem 150000 mpaka 200,000 hiyo ni mshamamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…